Msaada wa kisheria kufuatia ukiukwaji wa makubaliano ya kielectronic

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
Habari wanajamvi, naomba mnipe msaada wa hatua za kuchukua kwa mtu aliyekiuka makubaliano ya kibiashara. Mtu huyu ni rafiki yangu niliyefahamiana naye siku nyingi, alinihusisha kwenye biashara yake baada ya kujua kuwa i am better positioned kufanikisha biashara hiyo.

Bahati mbaya nilikuwa nje ya nchi wakati ananipa hiyo deal, hivyo mimi niliifanikisha bisahara hii nikiwa huko huko nje ya nchi. Kulingana na ukaribu wetu, hatukuingia kwenye mkataba wowote rasmi ila makubaliano yetu yalikuwa kwa njia za kielectronic yaani emails, simu na skype. Ushahidi wa makubaliano hayo toka mwanzo wa biashara hadi mwisho wa biashara ninayo katika format nlizozitaja hapo juu.

Nilipambana usiku na mchana kuhakikisha nafanikisha biashara hii kwa upande wangu kwani tulikubaliana anipe TZS 40M. Baada ya kumaliza biasahara, huyu jamaa alipokea hela yote toka kwa mteja aliyepo Tanzania na mimi sikuambulia kitu. Nimeshavumilia sana mana ni karibia mwaka sasa jamaa ananipa ahadi tu. Nadhani nimeshachoshwa na ahadi zake zisizokamilika.

Je katika mazingira ya namna hii mnanishauri nichukue hatua gani ili niweze kupata haki yangu???Ushauri wenu unahitajika ni matumaini yangu kuwa watanzania wengi wamekwisha kumbwa na dhurma ya namna hii hivyo elimu mtakayoitoa itasaidia watanzania wengi sana. Thank you in advance.
 
Back
Top Bottom