Mshati940
Member
- Apr 2, 2015
- 72
- 53
Niende kwenye topic moja kwa moja.
Katika harakati za kujikwamua kimaisha vijana kadhaa tukawa tumeingia mkataba wa kupangishwa nyumba na jamaa, mwenye nyumba. Na kama mjuavyo mikataba hii ya kawaida ya upangishaji mnasainishana mwenye nyumba, dalali na shaidi mmoja kama inavyofanyika maeneo mengi mjini Dar es salaam.
Ikiwa katikati ya muda wa mikataba yule mwenye nyumba akauza nyumba kwa mtu mwingine, mbaya zaidi akamuelekeza kwamba mikataba ya wapangaji wake inaisha muda ambao ni tofauti na mikataba halisi ya wapangaji waliopo.
Sasa mnunuzi mpya umefika muda alioambiwa anataka kuwaondoa wapangaji.
Je kisheria kipi kinaweza wasaidia wapangaji kupata haki yao maana muuzaji wa awali kwa sasa hapatikani na ajulikani alipo?
Naomba kuwasilisha