Msaada wa kisheria katika mikataba ya kupangisha nyumba na vyumba

Mshati940

Member
Apr 2, 2015
72
53
Niende kwenye topic moja kwa moja.

Katika harakati za kujikwamua kimaisha vijana kadhaa tukawa tumeingia mkataba wa kupangishwa nyumba na jamaa, mwenye nyumba. Na kama mjuavyo mikataba hii ya kawaida ya upangishaji mnasainishana mwenye nyumba, dalali na shaidi mmoja kama inavyofanyika maeneo mengi mjini Dar es salaam.

Ikiwa katikati ya muda wa mikataba yule mwenye nyumba akauza nyumba kwa mtu mwingine, mbaya zaidi akamuelekeza kwamba mikataba ya wapangaji wake inaisha muda ambao ni tofauti na mikataba halisi ya wapangaji waliopo.

Sasa mnunuzi mpya umefika muda alioambiwa anataka kuwaondoa wapangaji.

Je kisheria kipi kinaweza wasaidia wapangaji kupata haki yao maana muuzaji wa awali kwa sasa hapatikani na ajulikani alipo?

Naomba kuwasilisha
 
Frankie Lucas,

Siku zote wajinga ndio waliwao.

Hiyo mikataba yenu ilipaswa kushuhudiwa na Wakili/Kamishina wa Viapo au Mahakama ndio ingekuwa na nguvu za Kisheria. Kwa hapa ilipo hiyo 'mikataba yenu' siyo mikataba halali na halisi bali ni makaratasi tu ya kawaida kama yalivyo makaratasi mengine mnayoyafahamu.

Endapo kama mngekuwa na mikataba halali ya pango kati yenu ninyi wapangaji na huyo mwenye nyumba aliyeuza, mngeweza kumbana kisheria huyo mtu aliyenunua hiyo nyumba, yaani huyo mmiliki mpya wa hiyo nyumba.

Mngeweza kwenda Kwenye vyombo vya Sheria yaani Baraza la Ardhi la nyumba la Kata au Wilaya ili kumuwekea pingamizi asiweze kuwahamisha kwa nguvu mpaka hapo mikataba yenu halali ya Pango itakapo-expire.

Kwa kuwa mmeshalikoroga, msubiri kulinywa. Hizi ndizo gharama za ujinga!
 
Frankie Lucas,
Mkataba wako bado una nguvu kisheria, mabadiliko ya mmiliki hayana mashiko kuharibu mkataba wa awali.

Ilitakiwa mmiliki mpya angewaona na kuwaomba mikataba yenu ili aendelee na pale ilimpoishia na mwenye nyumba wa awali.

Bado sheria inakulinda kuwa na amani, usitoke mpaka muda wa mkataba utakapo isha, na kama huyo mwenye nyumba mpya anataka uhame akupe notes ili ujipange kuhama.
 
Wewe ni kilaza sijapata kuona... Kwahiyo makubaliano baina ya mwenye nyumba na mpangaji ni void yani haitambuliki kisheria ama? Hivi mlienda kusomea ujinga ama kujaza ujinga huko mashuleni, vitu vikiwa in written na kuna saini tayari mkataba huo unatambulika kisheria, huna akili wewe.
Mkuu all contracts are agreement but not all agreements are contract, ili mkataba uwe na nguvu kisheria unapaswa kuwa na sifa fulani, kuandikiana na kusainishana haitoshi kufanya uwe mkataba halali wa kisheria, ila kuhusu hii kesi nadhani hawa wapangaji wanayo nafasi ya kuweka zuio hadi muda wao utakapoisha.
 
Easy Chair Mark III, Mikataba ipo ya aina nyingi. Simple contract, speciality contracts. N.k na pia kuna sheria zinazosimamia sector mbalimbali.

Weka sheria inayotaka mikataba ya nyumba iwe sealed and attested sio kubwabwaja hovyo.
 
Mkuu all contracts are agreement but not all agreements are contract, ili mkataba uwe na nguvu kisheria unapaswa kuwa na sifa fulani, kuandikiana na kusainishana haitoshi kufanya uwe mkataba halali wa kisheria, ila kuhusu hii kesi nadhani hawa wapangaji wanayo nafasi ya kuweka zuio hadi muda wao utakapoisha.

Mwambie huyo Na LLB yake uchwala

Bush Lawyers
 
Wewe ni kilaza sijapata kuona... Kwahiyo makubaliano baina ya mwenye nyumba na mpangaji ni void yani haitambuliki kisheria ama? Hivi mlienda kusomea ujinga ama kujaza ujinga huko mashuleni, vitu vikiwa in written na kuna saini tayari mkataba huo unatambulika kisheria, huna akili wewe.
Nadhani jamaa hajui kitu kuhusu sheria maana huyo mmiliki mpya ndo anatakiwa apate kibali cha mahakama ili awaondoe hao wapangaji kwa nguvu.
 
Mkuu all contracts are agreement but not all agreements are contract, ili mkataba uwe na nguvu kisheria unapaswa kuwa na sifa fulani, kuandikiana na kusainishana haitoshi kufanya uwe mkataba halali wa kisheria, ila kuhusu hii kesi nadhani hawa wapangaji wanayo nafasi ya kuweka zuio hadi muda wao utakapoisha.
Kimsingi hao ni wapangaji licha ya mapungufu ya mikataba yao hivyo taratibu za kuwaondoa kinguvu ni mpaka mahakama itoe kibali.
 
Wewe ni kilaza sijapata kuona... Kwahiyo makubaliano baina ya mwenye nyumba na mpangaji ni void yani haitambuliki kisheria ama? Hivi mlienda kusomea ujinga ama kujaza ujinga huko mashuleni, vitu vikiwa in
written na kuna saini tayari mkataba huo unatambulika kisheria, huna akili wewe.
Japo Mimi ni 'saveya ' umeandika vizuri ila mwishoni umeharibu Kwa kusema hivi "vitu vikiwa in written na kuna saini tayari mkataba huo unatambulika kisheria " hapa umekosea Kwa sababu sio kila makubaliano yote sio mikataba hebu soma kifungu cha 10 cha sheria ya mikataba, halafu ulitakiwa umuulize swali kama hiyo ardhi imepimwa na kusajiliwa?

By the way sheria ya ardhi inaruhusu kuuza nyumba ikiwa na 'lease ' Kwa maana obligation za previous leasor zinahamia Kwa new landlord
 
Back
Top Bottom