Msaada wa kisheria juu ya mgogoro huu wa ardhi

Ayenda M

Member
Jan 4, 2018
97
132
Habari wadau,

Ni mwaka sasa tangu mzee wangu anunue ardhi kutoka kwa mzee mmoja ambaye alikuwa jirani yetu. Mara tu baada ya kukamilisha hatua zote za manunuzi na nyaraka zote kusainiwa kila kitu kilionekana shwari.

Siku tatu baada ya mauzo aliibuka kijana wake ambaye alidai shamba lile ni mali ya marehemu mama yao na baba ameuza mali zao. Shauri hilo lilipelekwa mahakamani na baadae kwenye baraza la ardhi, mwisho wa siku mzee wangu (mnunuzi wa ardhi) alishinda shauri hilo.

Ila nimefika hapa home, nimekuta dogo aligoma kuvuna mihogo yake mwaka na nusu sasa anadai kuwa atavuna siku akipenda. Nimemuita na kuongea naye kikubwa japo sijui sheria ila kagoma na kusema mihogo yake ibaki na ataivuna siku akijisikia kufanya hivyo.

Nimekuwa na mawazo ya kuivuna mimi kama mimi na kuitumia kwa matumizi ya familia ila mzee wangu anaogopa baadae kuja kutokea baadhi ya masuala kadhaa. Mimi ninazo sababu za kufanya hivyo kwa sababu ni mwaka na nusu sasa,

a) Shamba tunamiliki sisi.

b) Palizi na masuala mengine yote tunafanya sisi yahusuyo shambani mazao. Vipi sasa yeye atapata wapi haki ya kuja kuvuna na kufaidika na kitu asichokihangaikia na kujua matunzo yake yapoje?

Je, nikiamua kuvuna mihogo hiyo kuna shida yoyote ya sheria ya ardhi inaweza kunipata kutokana na ukweli kuwa ni mwaka na nusu sasa tangu shamba lile halali yetu na shughuli zote tunafanya sisi.

Wajuzi wa sheria ninaomba msaada nifanye nini?
 
Kwa kweli ni mtihani,mimi pia nilinunua shamba na mazao yake cha ajabu mtoto wa muuzaji bado anavuna mazao yale na kuuza kwa ushahidi wa majirani, tumeenda kumuonya hatuku mkuta tukaacha ujumbe.Je wewe katika mauziano huku nunua na mazao?
 
Unachotakiwa kufanya ni kuwasilisha shauri la utekelezaji wa hukumu uliyoisema iliyompa ushindi Mzee wako kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya uliyopo.

Utekelezaji ni pamoja na kuondoa chochote ambacho si mali yenu kwenye eneo husika(hiyo mihogo). Hivyobasi,Baraza litamuagiza mwenye mihogo aiondoe mihogo yake kwa muda maalum atakaopewa. Kindly be advised.
 
Kwa kweli ni mtihani,mimi pia nilinunua shamba na mazao yake cha ajabu mtoto wa muuzaji bado anavuna mazao yale na kuuza kwa ushahidi wa majirani,tumeenda kumuonya hatuku mkuta tukaacha ujumbe.Je wewe katika mauziano huku nunua na mazao?

Nasi pia tulinunua na mazao. Ila dogo anakomaa eti mihogo ilikuwa yake na atavuna siku akiamua. Usumbufu mtupu
 
Unachotakiwa kufanya ni kuwasilisha shauri la utekelezaji wa hukumu uliyoisema iliyompa ushindi Mzee wako kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya uliyopo. Utekelezaji ni pamoja na kuondoa chochote ambacho si mali yenu kwenye eneo husika(hiyo mihogo). Hivyobasi,Baraza litamuagiza mwenye mihogo aiondoe mihogo yake kwa muda maalum atakaopewa. Kindly be advised.

Shukrani sana mzee! Hili wazo sikuwa nalo, nalifanyia kazi.
 
Nasi pia tulinunua na mazao. Ila dogo anakomaa eti mihogo ilikuwa yake na atavuna siku akiamua. Usumbufu mtupu
Ardhi ni mali yenu kutokana na mkataba wa mauziano,hakuna haja ya kubembelezana tumia ubabe...kama mnataka muanze ujenzi msikwamishe na mpuuzi mmoja.

Mpe notice ya siku saba....hataki vuneni muendelee na mambo yenu.Ila mjiandae kwa lolote anaweza tumia njia za giza
 
Back
Top Bottom