Msaada wa kisheria juu ya haki yangu kwa mtoto

BABA LEA WATOTO

JF-Expert Member
May 6, 2017
338
722
Kuuliza ni kutaka kujua ama kupata ufafanuzi, ninakusudia kwenda mahakamani kuomba haki ya kuweza kumuona ama kutembelewa na mtoto wangu (binti wa miaka mitano) baada ya kutengana na mama yake.

Iko hivi baada ya mgogoro wa muda mrefu tuliamua kwa hiari yetu kutengana huku tukijiandikia makubaliano juu ya mtoto kwa kipindi chote akiwa chini ya miaka saba, ambapo mama wa mtoto alipata haki ya kuishi na mtoto huku mimi nikilipa ada ya shule na mahitaji mengine nitakayopenda kutoa, pia nilimwachia vitu vyote vya ndani kama sehemu ya huduma kwa mtoto huku nikipewa haki ya kumwona mtoto pale ninapohitaji.

Mgogoro ukaanza pale ambapo mzazi mwenzangu hapendi mtoto aje kwangu anapokuwa likizo, nikimwomba mtoto matusi na malumbano yasiyokoma, nikaona niende ustawi wa jamii, huko ikaamuliwa kwamba mtoto atakaa na mama wakati wote wa shule na atakaa kwangu wakati wa likizo zote, cha kushangaza kinyume na makubaliano amenigomea mtoto na amempeleka kwao kipindi hiki cha likizo, nimeamua kurudi tena ustawi wamemwambia afuate makubaliano husika, yeye hayupo tayari na anasema maamuzi yanamkandamiza bora nimepeleka mahakamani.

Ombi langu, nataka niende mahakamani, je nidai access ya mtoto ama kuishi na mtoto kabisa lipi ni sahihi kwa mazingira haya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana kwa yanayokusibu bestie kisheria mtoto chini ya miaka 7 anatakiwa kukaa kwa mama yake, baada ya hapo utaamua umchukue au umwache kwa mama yake.

Kulingana na maelezo yako inaonekana wazi mke wako ni jeuri mno, kama anataka uende mahakamani nenda tu mpendwa ila liko wazi maamuzi hayatokuwa tofouti na ustawi wa jamii.

Mwisho kama bado upo single na unahitaji kuwa na mtu Pm yangu ipo wazi bestie kila la kheri

Aisee na mimi naruhusiwa ku PM?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom