GIPAMA
JF-Expert Member
- May 21, 2016
- 1,103
- 541
Ndugu wana bodi, amani na iwe kwenu...... Nimetatizwa na jambo hapa naomba kusaidiwa kiushauri.....
Nitasema bayana ili nieleweke wazi......
Mimi bana ni kijana(29yrs), kuna dada mmoja japo ameolewa na ana watoto wawili........ Sasa alitokea kunipenda na kunitega kwa kila namna kila nikikutana nae mara aniambie:-
*nimependeza,
*mara kiharufu cha mwili wangu ni kizuri anatamani kukisikia kila muda,
*mara mimi ni mtanashati na vingine vingi sana hadi vizawadi kidogo.....
Nami nna stress zangu kama mhanga wa ajira nikaona isiwe tabu, nikamtest kumuomba namba naye akanipa, akanipangia mida ya kuwa tunachart..........
Tukachart mpaka kujikuta tupo kwenye mahusiano na akafanya ujanja siku moja akaaga anaenda safarI tukalala nae sehemu mpaka asubuhi.....
Shida ni kwamba, tumeendelea kuwasiliana nae na kukutana kwa usiri mkubwa, ila JUZI mumewe akamkwapua simu kipindi anachart na mimi na kuzikuta sms zetu tunazochart..... Akanyang'anywa simu mpaka dakika hii hana simu.
Leo kanitafuta ana kwa ana akanambia mumewe aliita wazazi wake, yaani wazazi wa mwanaume na kutaka amkatae mwanamke kuwa aende kwao, lakini wakaongea ongea yakaisha.
Tabu ikaja kwa makubaliano yaliyofanyika kati ya mzazi na mume mtu ya kwamba, waipeleleze ile namba ni ya nani, ambayo nilikuwa naitumia kuwasiliana na mwanamke huyo( namba yangu mimi) ili wakishamjua mmliki wake waende kumshtaki kwa mtendaji........ Kuanzia hapo wananibeep kwa kutumia line ya mwanamke ila sipigi simu maana nmeshatonywa.
Swali langu ni je, kama jamaa atanigundua na hajanikamata, ila akagundua mwenye ile namba ni nani? Je hii itampa nguvu kisheria kwenda kunishtaki?
Je kama akinishtaki kwa mtendaji, atanishtaki kwa kosa lipi kisheria? Maana sijatuma sms za matusi..... Pia mwanamke alinikana kuwa hanijui na hajui huyo mtu anaemtumia sms ni nani......
Hiyo imekaaje kwenu wajuvi wa mambo? Asanteni.