Mm ni mfanyakazi katika tasisi moja hapa Dar es salaam nimefanya kazi katika tasis hii miaka 2 ba miezi sita, niliahidiwa kupewa mkataba ila ilichukua takribani mwaka mzima pasipo kupewa mkataba kila napodai naapiwa nitapewa nilivyoona muda unazidi kwenda basi nikaomba nipewe salary slip ila bado nilijibiwa ovyo na na wenye mamulaka, nikaenda tena kuulizia vipi pesa yangu ya NSSF napo nilijibiwa sikupewa jibu miaka miwili bila kulipwa pesa ya NSSF, baada ya mwaka mmoja nikaitwa kupewa mkataba amabo uliandika nusu ya mshahara wangu(besic salary) amabao ulionyesha masaa ya kazi ni masaa 11, nikauliza kwa nn mshara(besic salary)yangu imeandikwa nusu nakuandika ndo mshahara wangu wote kwa mwezi wakaidai eti ni kukwepa kodi ya serikali nikawaambia sasa hamuoni tunafanya kwa kuhujumu uchumi wa Tanzania maana hapo mnakwepa kodi ya serikali, baada ya kusema hivyo nikatishiwa kuachishwa kazi kwa kuwa na mimi sina chochote na familia inanitegemea nikaogopa kufukuzwa ikabidi nisaini ule mkataba feki nikiambiwa nisiwe na wasi wasi kodi ya serikali inalipwa, na nikakazwa kutoka inje na ule mkaba niliomba sana ili nije inje nitafute msaada ila walikataa na kudai nisaini niache pale pale, nikaendelea kufutilia nipewe kopi ya ule mkataba ila bado niliendelea kunyima na kuniona mimi kama adui wa tasisi walidai na hamasisha wengine. Mwanzoni mwa mwezi huu saba wameniterminate. Pasipo kupewa mshara wa mwezi wa tano, wa sita na wa saba na haki zangu zingine ninazostaili km mtumishi wao. Naombeni msaada wanasheria humu ili niweze pata haki zangu.