radika
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 20,427
- 32,196
Bila kupoteza muda niende kwenye mada.
Dada yangu na mume wake walinunua nyumba dodoma maeneo ya Nkuhungu ambayo waliuziwa na mdogo wa mwenye nyumba basi katika hayo mauziano alikuwepo wakili wasonga maarufu sana hapo Dodoma na Mwenyekiti wa kijiji kama shahidi na kulisimamia hilo zoezi.
Baada ya kama miaka kama mitano kupita aliibuka dada wa marehemu na kusema kwamba alieuza nyumba mdogo wao wa kiume hana mamlaka hayo na amelaghaiwa ktk kuuza kesi ikaanza ktk mabaraza ya kata ndipo wakina dada wakaomba aletwe ndugu yao aongee au aonekane jambo ambalo walipinga ndugu wa muuzaji kwamba hayupo kapotea.
Baada ya kuhangaishana sana walianza kutembeza rushwa ndipo waliposhinda kesi na dada yangu kushindwa na inasemekana mumewe na huyo dada yupo serikalini alikuwa akitumia hiyo fursa.
Dada alikata rufaa mahakamani bado hukumu zilitoka kama mwanzo maana michezo ilianza toka katika mabaraza ya ardhi ya kata wazee wa mabaraza tayari walikuwa wanajua nini cha kufanya.
Ilifika kipindi wakili wasonga alijitoa ktk kesi kwamba kesi imekuwa ngumu kwao wakati ktk mauziano ya nyumba alishiriki na kukagua hati za mauziano za nyumba na hata kubadili umiliki wa nyumba kwenda kwa dada na mumewe na allikuwa akilipwa kila hatua gharama za huduma yake.
Lengo langu naombeni msaada dada yangu alitolewa ndani ya nyumba na nyumba ikauzwa haraka sana.
Pia naweza nikawa sijatoa maelezao ya kunyooka sana kama kuna atakae hitaji kumsaidia kisheria na ushauri namba zake ni hizi.
0712 505 872