Msaada wa kisheria baada ya Makubaliano ya Matunzo ya mtoto

Mbutuka

Member
May 26, 2010
16
1
Naomba msaada kwa wanasheria. Nimezaa na binti ambaye hatukuweza kuoana kutoelewana kuhusu dini zetu. Aliwahi kunishauri tufunge ndoa ya serikali lakini kutokana na imani yangu hii ndoa haikubaliki. Niliendelea kutoa matunzo kwa huyo mwanamke tangu alipokuwa mjamzito hadi amejifungua. Baadae niliamua kuoa ndipo kasheshe zilipoanza. Akaenda ustawi wa jamii, tukafanya makubaliano ya kumlea mtoto kisheria. Lakini kila siku haishi vituko, mara adai anataka alipiwe kodi ya nyumba, mara nimlipie mfanyakazi anayekaa na mtoto vitu ambavyo ustawi wa jamii hawakukubaliana navyo. Sasa ameamua kunichafua, kwa kunitangaza vibaya kwa mitaani na imefikia hatua hata kuja ofisini na mtoto. Kwangu naona ananidhalilisha kwa kuwa kama ni matunzo ya mtoto mimi napeleka ustawi wa jamii tena kiwango mara tatu ya kile kinachotakiwa kisheria. Naomba wanasheria mnisaidie nifanyeje kisheri ili kukomesha tabia hiyo.
 
Tatizo linaonekana sio matunzo ya mtoto, ila pia na kuwin maisha.
Kuzaa bila kuolewa kunaonekana pia kumemkatisha tamaa na maisha.
Anaamini kuwa mwanaume ni njia ya kuwini maisha.
Jaribu kujiweka katika nafasi yeke then utaona kuwa yuko desperate.
Mkae muongee, ikiwezekana akukabidhi mtoto umlee mwenyewe
kama anaona anamletea kiwingu.
 
Back
Top Bottom