Msaada wa kisheria: Afisa elimu wa Bagamoyo amezuia mshahara wangu

mbeyaman

Member
Sep 28, 2013
97
28
Mimi ni mtumishi katika idara ya elimu Bagamoyo.

Nilikwenda kusoma baada ya kukataliwa releasing letter, mshahara umezuiwa kwa muda mrefu, niko kazini still mshahara wangu umezuiwa.

Naombeni ushauri ili nipate haki zangu.
 
Wewe hujapewa ruhusa ya kwenda kusoma kwa maana nyingine wewe ni mtoro kazini, sasa unataka msaada gani wakati huna ushaidi kwamba muajiri alikuruhusu ukasome! Hiyo imekura kwako kisheri wewe una makosa hapo hamna msaada wa kisheria labda uangalia njia nyingine.
 
Mimi ni mtumishi katika idara ya elimu Bagamoyo.

Nilikwenda kusoma baada ya kukataliwa releasing letter, mshahara umezuiwa kwa muda mrefu, niko kazini still mshahara wangu umezuiwa.

Naombeni ushauri ili nipate haki zangu.
Uliondoka bila ruhusa, umerudije kazini? Uliripoti kwa mwajiri wako na kukupangia kazi au ulirudi kimyakimya na kuanza kazi?
 
Ulifanya kosa kuondoka bila ruhusa. Kusimamishwa mshahara ni hatua stahiki kwa kosa lako. Hajakosea kitu hapo.
 
Mimi ni mtumishi katika idara ya elimu Bagamoyo.

Nilikwenda kusoma baada ya kukataliwa releasing letter, mshahara umezuiwa kwa muda mrefu, niko kazini still mshahara wangu umezuiwa.

Naombeni ushauri ili nipate haki zangu.

ni halali yako kabisa ulitaka ule mshahara bila kufanya kazi
 
Kuna mwalimu naye alipatwa na tatizo kama hili, yeye alikuwa na ruhusa ya kwenda masomoni ila alipomaliza hakuripoti kazini kwa mwaka mzima. Walimfungia mshahara kwa miezi mitano. Baada ya kujieleza sana na utetezi wa mkuu wake wa shule, hatimaye wameendelea kumlipa.
 
Ushauri wangu kwako rudi kwa mkuu wako ukiwa mpole, mwombe muongozane naye kwa Afisa elimu wako, muongee huku ukijua wewe ni mkosaji. Inawezekana uliondoka mkiwa tayari hamuelewani, ni muda sasa wa kuwa mpole as you can. Ila ukianza hivi kutafuta msaada wa kisheria naamini itakula kwako, jamaa watakufungulia chaji (kama bado) then wataku-fire kabisa.
 
Pia hakuna sheria inayosema, ukienda kusoma unyimwe mshahara hata bila release letter. Wao inatakiwa wafanye taratibu zote za kukufukuza, kwa nini wameshindwa kufanya hivyo? Washindilie labour utawashinda
 
..mhh hii imeangukia pabaya haloo! hizi enzi za awamu ya tano wanatafuta watu kama nyie wa kuwaoshea ili waonekane wapo kazini, nakushauri wahi mapema kwa huyo afisa elimu wako mkaliweke hilo sawa kabla hawajahamishwa..kuna panga pangua itapita muda si mrefu ya wakuu wa idara halimashauri zote, manispaa na majiji kama ilivyokua kwa ma-DC na DED
 
Back
Top Bottom