Msaada wa kisaikolojia: Mtu anaependa kukaa mwenyewe

mi ndo addicted kabiss na kukaa peke angu..had sasa nachukia kukaa ndani ya nyumba yenye watu wengi..nataman ningekua na kaz nkapangishe room yangu mbali huko nkae pk angu..napenda kula pk angu.kulala pk angu..hata darasani sec na chuo sikuwa na makundi..tufanye kaz za group tukimaliza mi fyuu!!kwenye kiti changu. sitaki usumbufu.home mda mwingi najiskia comfortable kukaa room kwangu kuliko nje!
 
I enjoy being alone or with few people wasizid wawili tena ninaowakubali sio kujichanganya changanya hovyo hovyo,nkishamsalimia mtu basi kila mtu ashike hamsini zake sitaki kujua mambo ya mtu na sitaki mtu kunijua jua unless nijisikie mwenyewe
Uuuuwiii thats me! Yaani yote uliyoyasema ni kama yangu!
 
Kweli kuka peke ako aimanishi ujiamin au unogopa au unaona aibu la hasha!mi bana sina aibu n wala siogop tena linapokuja suala la kunikwaza au nikuambie ukwel kuhusu jambo ambalo naliona haliko poa.. Wee lazma utashngaa ndo huyu anayekaaga kimya au! ....nakupa makavu yako tu den story zinaendelea
Hata mie siweki kitu moyoni mtu akizingua
 
Mi hata mtu akitaka urafiki siukubali, mpaka niuanzishe mimi.

Watu wenyewe hawaeleweki then ukae unafuatanafuatana na mtu ambaye zaidi atakupotezea muda wako. Hata sasa niko mwenyewe nyumbani kimya. Mtu akipita nje ya geti anaweza dhania hakuna mtu.

Kuna faida nyingi za kuwa hivi ingawa hasara yake naona ni UCHOYO na KUJIONA KUWA UKO SAHIHI KWA KILA JAMBO maana mtu unakuwa umezoea KUWA mwenyewe mwenyewe KWA MUDA MREFU.

hahahaha upendagi ujinga kabisa!
 
Bwana mwenyewe hata mimi nina hilo tatizo kama siyo tatizo nina hiyo tabia, lakini tumetofautiana kidogo; mimi napenda kuishi na watu hata nikiwa sehemu tofauti napenda kujichanganya na watu ingawa huwa siyo mzungumzaji mkubwa always huwa mtulivu ninayependa kusikiliza. Kama walivyo wengine bwana mwenyewe hata mimi sipendi kelele, nakumbuka wakati bado nipo nyumbani usiku nilikuwa silali mpaka wengine watakapomaliza kufanya shughuli zao kwa sababu nilikuwa sipendi kelele. Mimi hata kula napenda kula mwenyewe, bwana mwenyewe napenda kufanya mambo yangu mwenyewe tena kimya kimya.
 
Tuko wengi bila shaka. Jamii ina mitazamo yake. Mfano, wengi wanadhani kuwa uongeaji sana ndio the best ideal personality. Lakini ukweli ni kuwa, dunia inahitaji kila aina ya watu. Na kwa sisi tulio wakimya na tusiopenda makundi, hilo wala si tatizo. Kuwa hivyo si kwamba una matatizo. Ni mojawapo tu ya AINA za binadamu. Ni kweli kuna wakati inaweza kuwa tatizo, lakini hata uongeji ukizidi nao unaweza kuwa tatizo. Mara nyingi tulio wakimya TUNAFIKIRI sana. Maisha yetu kwa kiasi kikubwa yanaendelea ndani kwa ndani. Usijilaumu kwa kuwa mkimya. Kuna faida zake (japo wengi hawatuelewi na wanatutafsiri vibaya).
 
Nami mmoja wapo..sipendi kelele kabisa yani nikikaa sehemu nikaona watu wanapiga story ambazo hazinipi faida yoyte ile lazima ntanyanyuka maana mwisho wa siku tutaishia kusengenya...napenda sana nikiwa peke angu hata kwenye swala la kuangalia movie basi niangalie mwenywe au kama yupo mtu pemben yangu basi mawazo yetu yawe pamoja..sio mim nasikitika au nachka kuhusu movie we unaaza maswal unacheka nin!!....pia nadhan inanisaidia kuepuka na vitu vingi tu mfano ugomvi au marumban yasonatija...napenda kukaa peke angu nikiangalia movie..kusoma vitabu au kupeluzi kwa simu ili kujua nin kinaendelea dunia..lakin ukinifta nilipo na tukapiga story mdgomdgo hapo sawa ..ila tu usiwe mtopokaji wa ovyo!!....KUPITIA IVYO NAJIONA MWENYE FULAHA NA AMANI KULIKO KUKAA NA WATU WENGI ALAFU WAKAICHOSHA AKILI YANGU
Mkuu tunaendana sana mimi mpaka nyumbani huwa hawnielewi ila ndo niko hivyo niko kama wewe , sitaki ujinga ujinga nikiona watu wanaongea au kufanya mambo nisiyoyaapreciate naondoka naenda kukaa mbali
 
Tunaopenda kukaa kimya tunapenda kukaa wenyewe huwa tunatafsiriwa tunajisikia ila sio hivyo
 
Ukikapenda kukaa mwenyewe uwe unafanya vitu vya msingi, sio kuangalia porn ohoooo
 
Mi hata nikikaaga n mtu huwa sina story. Mpka mwnywe aanzishe na majib ni mafup mafup tu. Huwa siko confortable tukibaki sehem wawili tu ntatafta sababu ya kutoka au labda aongezeke mtu mwingne ili wao waweze kuongea
 
Sifa zetu ni hizi
1 ni vigumu kuwa chama cha CCM
2 atuendiendi kwenye nyumba za ibada
3 atupendi mambo ya kinafiki
4 ufikili kwa kutumia akili
5 atupendi kusumbua mtu wala kusumbuliwa
6 atupendi kujionyesha kipumbavu
Hata ni baadhi tu

Umepatia kabisa. Ila la 2 kwangu ni opposite.
 
Mimi nikienda sehemu ama nikiwa ugenini siku mbili au Tatu naweza kukaa kwenye watu zaidi ya wawili lakini baada ya siku 3 kuisha hata kusikia sauti yangu ni bahati Yao Hua nashinda mwenyewe tu siwezagi kukaa kwenye kalele,, siku mtaa wetu kukiwa na sherehe lazima nitengeneze safari ya dharura mimi na kalele ni kama simba na swala mikumi
 
Back
Top Bottom