Msaada wa kimawazo unahitajika....nimeshindwa kumuelewa huyu mrembo

Oct 21, 2010
13
0
....Nimetokea kumhusudu...tunafanya naye mazoezi kila w/end.....pia tunajumuika katika mitoko mbalimbali....ni msichana mrembo, kaumbika, anakazi yake na msomi.... lakini nashindwa kumuingia sababu nimedokezwa na rafiki yake anayemfahamu kwamba hana msimamo wa kimapenzi, hajatulia....anawanaume tofauti ikiwemo waume za watu na bado anajipendekeza niwe naye.....sasa sielewi anachotaka ni nini maishani....anaonyesha anapenda awe na mtu wake atulie maishani, lakini nawasiwasi kama anaweza kuhimili ups and downs za maisha bila kumtegemea mtu.....mpaka inanipelekea ku-conclude kwamba huenda anatafuta mtu ambaye atamtoa kimaisha, anapenda kulelewa kuliko kutafuta chake mwenyewe kwa kujigonga kwa wanaume wanaoweza kumhonga....hivi jamani kuwa na mtu kama huyu maishani si mzigo....maana sidhani kama atakuwa na uaminifu, ikitokea shida atakimbilia kwa wanaume badala ya kusimama na ku-fight na mmoja ampendaye.....

naombeni ushauri wenu...nimpe somo la maisha huenda atabadilika...au nimshit tu nimwache kama alivyo tubaki tuwe marafiki.....maana miaka inaenda kwa binti mzuri kama huyu...atababaika na wanaume na wasimfanyie chochote cha maana....akifikisha miaka 35 ndo uzee unakuja alafu hujapiga hatua yoyote hamna mwanaume atakayetaka kuwa naye tena....
 
unajuaje huyo rafiki yake alikuwa anamzushia tu?...anamuwekea kauzibe ili akupate?
 
fanya utafiti wa kina kwanza mkuu kabla ya kuhitimisha.na kwavile mnakua pamoja mara kwa mara then itakua sio kazi sana kwako kufanya utafiti wa kina.
 
kaka kama vipi we unga nae ila jitaidi kumbadilisha izo tabia zake ukiona bado achana nae kabla ujazama kabisa
 
what u have to do ni kumchunguza kiundani zaidi kama ni kweli tabia hiyo anayo kama kweli anayo na kakutamkia kua kakupenda basi muulize jee tutakapo kuwa pamoja utawacha tabia ulioyonayo akikana kua hana tabia yoyote basi ni fika atakua ni msiri na kutokua muazi na itakapo timiza haja yake ya kuwa nawe basi kaa ukijua fika huyo hatakufaa na ataendelea na mambo yake chini chini ila akikwambia ukweli na uwazi basi jua kwamba keshajiaminisha kwako wewe arbab,,,
 
kutambua undani na tabia ya mwanamke ni jambo gumu sana. Jitahidi lakini
 
Fab....sio kwamba sijafanya uchunguzi....tena baadhi yao nimeshawaona katika ile tokatoka yetu, na utakuta anawaponda jinsi walivyo.....na sasa huyo mmoja ambaye ni mume wa mtu ndie anachat naye kila saa....mpaka majina nayajua....huyu rafiki yake ametulia, anamtu wake, tena anachotaka ni kumuona huyu rafiki yake ampate mtu wa kutulia naye....maana siku zinakwenda....
 
Fab....sio kwamba sijafanya uchunguzi....tena baadhi yao nimeshawaona katika ile tokatoka yetu, na utakuta anawaponda jinsi walivyo.....na sasa huyo mmoja ambaye ni mume wa mtu ndie anachat naye kila saa....mpaka majina nayajua....huyu rafiki yake ametulia, anamtu wake, tena anachotaka ni kumuona huyu rafiki yake ampate mtu wa kutulia naye....maana siku zinakwenda....

kuna wanawake sio 'wife material'...kwa jinsi ulivyoelezea huyu mwanadada anaangukia kundi hili,chapa mwendo ndio ushauri wangu.....tafuta mwingine,sidhani kama utaweza kumbadilisha kama kufikia umri huo hajataka mwenyewe kubadilika.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom