BALIMI CASTLE
Member
- Aug 2, 2017
- 33
- 47
Kuna auncle wangu mmoja alimaliza form six mwaka 2013,alisoma PCB,matokeo yake yalikuwa PHYSICS (S) CHEMISTRY (E) BIOLOGY (D), alipata nafasi ya kuajiriwa sehemu flani hivi, akasema ataenda kusoma badae,kweli akafanya kazi Mpaka 2018 akaona arudi shule Sasa, lakini akakuta principle pass moja imepungua, kwa maana miaka ya nyuma ilikuwa ni EE unapata chuo, alikwenda open university wakamwambia asome foundation course mwaka mmoja then atasoma degree, lkn Akanambia kuwa masomo ya foundation course ni yale yale ya advance tena unayarudia kusoma yote, akaona kupoteza muda kusoma masomo ya advance kwa nini asirisiti somo moja tu ili apate principle pass, ukiangalia baadhi ya masomo Kama biology alikuwa amefaulu.Akawaza somo gani Sasa alifanyie mtihani? physics akaona atapoteza muda, kwa sababu aliona halimudu hivyo angetoka patupu, kama Mara ya kwanza alipata S, alijua Mara ya pili angepata F.hivyo akaliacha,akawaza chemistry, nayo akaona mazingira sio Rafiki kwake, kwa kuwa sehemu alipo kumpata mwalimu wa chemistry ilikuwa ni vigumu, Hivyo akaona kuwa atapoteza muda tu, solution ikaja akaona asome geography,ili atoke kwenye PCB aje kwenye CBG,kweli akasoma geography kwa miezi 8 tu akafanya mtihani wa form six mwaka huu, matokeo yametoka Jana ameniambia amepata principle pass grade D, Sasa kuna chuo alikuwa anafanya registration online kw kuwa amekusuduia aombe nafasi ya kusoma hapo,amejaza vizuri education information kuanzia form four hadi six, tatizo likajitokeza pale kwenye kujaza second seating ya advance, alipojaza namba yake ya mtihani na kituo na mwaka aliomaliza( 2019) kisha kusubmit,sytem ilimwambia second seating hai match na CSSE record, je kubadili hilo somo inaweza kuwa reason? Yani kutoka PHYSICS to GEOGRAPHY.je kunaathari kwa alichofanya? Maana anasema Alicho zingatia mwanzo ni kuona, anaweza kusoma course flani kwa kuwa ilitaka principle pass ya geography na biology. mwenye uelewa tafadhali.