msaada wa kimawazo kwa mke wangu amepata ujauzito wa kumfatisha mtoto wetu wa pili

Zungweboy

JF-Expert Member
Jun 10, 2018
363
178
Habari wadau za muda huu,

Mimi nafamilia ya watoto wawili na mke mmoja.

Mke wangu kapata ujauzito wa kumfatisha mtoto wetu wa pili.

Tatizo si kumfatisha tatizo kumfatisha mtoto akiwa na mwaka mmoja.

Tena alimpata kwa njia ya upasuaji mkubwa.

Hofu yangu je mke wangu atalajie kujifungua kwa upasuaji tena?

Na hadi muda huu mtoto afya yake sio nzuri.

Kwasababu mtoto alikua ameshatembea lakin sasa ivi hatembei wala kutamba kwa ufupi hali yake sio nzuri.

Je, nitumie njia gani kurudisha afya ya mtoto kwa haraka zaidi?

Toka mwezi wa 12 mwaka jana sipo vizuri kisaikolojia hadi sasa, nimejawa na mawazo kwa kiasi kikubwa juu ya afya ya mama na mtoto
Msaada wenu wadau kwa mawazo yenu pevu
 
Ushauri wangu ambao si wa kitaalamu, kama bado anamnyonyesha mtoto aache mara moja, ila mkazanie kumpa lishe bora, mazoezi na kama ana homa homa mpelekeni kituo cha afya kwa matibabu zaidi, ila muhimu kwa huyo mtoto wa mwaka mmoja ni lishe bora atarudi kua sawa.

Kuhusu mkeo kujifungua tena kwa upasuaji hilo halikwepeki.

Mola awanusuru.
 
Unatakiwa ujue kuwa ukishazaa kwa Operation, inatakiwa walau ukae hata miaka mitatu ndo uzae tena, Miaka mitatu ni mda unaotelewa kuhakikisha lile kovu la kizazi linakua imara kubeba mtoto mwingine.

Ifahamike kovu likiwa legelege uwezekano wa kupasuka kizazi ukiwa na kovu kwenye kizazi ni mkubwa sana especially kama haujafika hiyo miaka mitatu.

Ukishazaa kwa Ceasrian Section, chances zinabaki kubwa kwa practice ya Tanzania tena kuzaa kwa kisu. Hakuna anaetaka ku risk ku monitor mtu ambae ana chances za kupasuka Kizazi.

Kufupisha story, by standard Mke wako anatakiwa azae tena kwa kisu.

Hayo ya mtoto mpeleke kwa daktari wa watoto amu evaluate, usijekuta ana matatizo mengine ambayo yanamfanya anashindwa kukua.

Failure to thrive au Delayed Milestones ni ishara mtoto anashida nyingine ya kiafya inayotakiwa kuchunguzwa.

EDIT/Nyongeza: Usiwe taken up na Socoety beliefs sijui za kubemenda na takataka zinazofanana na hizo, mtoto wako anaumwa trust me, mpeleke kwa Daktari amu evaluate.
 
Unatakiwa ujue kuwa ukishazaa kwa Operation, inatakiwa walau ukae hata miaka mitatu ndo uzae tena, Miaka mitatu ni mda unaotelewa kuhakikisha lile kovu la kizazi linakua imara kubeba mtoto mwingine.....
Asante sana.

Imetokea tu alikua anatumia njia ya uzazi wa mpango (vidonge).
 
Back
Top Bottom