Msaada wa kiafya wana jamiiforum

mbiligenda

Member
Dec 3, 2015
87
48
Habari za asubuhi wapendwa,

Nimeamka nikiwa na maumivu makali sana kwenye sikio la upande wa kushoto,nimejaribu kutoa uchafu lakini maumivu bado yanaendelea,kabla sijaenda kwenye kituo cha huduma ya afya,mwenye utaalam kidogo anisaidie hata kwa ushauri,dawa au huduma ya kwanza,karibuni!
 
inawezekana una infection kwenye sikio, kuna ear drops zinaitwa sodium bicarbonate eardrops jaribu kutumia zitatibu hilo tatizo ila kwa ushauri zaidi fika kwa daktari.
 
Habari za asubuhi wapendwa,

Nimeamka nikiwa na maumivu makali sana kwenye sikio la upande wa kushoto,nimejaribu kutoa uchafu lakini maumivu bado yanaendelea,kabla sijaenda kwenye kituo cha huduma ya afya,mwenye utaalam kidogo anisaidie hata kwa ushauri,dawa au huduma ya kwanza,karibuni!

Huu muda uliopoteza kuandika ungeenda tu pharmacy hapo jirani au hata Hospitali ya karibu nawe ungeshapona kitambo. Na sidhani kama kweli unaumwa Sikio Wewe kwani kwa maumivu makali ya Sikio hakyanani hata usingethubutu ku log in huku!
 
Sikio ni kiungo sensitive sana usichokonoe na chochote wala kuweka dawa yoyote nenda hospital mapema kamuone mtaalamu wa masikio waangalie kuna nini ndani upewe dawa kwa dar es salaam AAR posta au magomeni karibu na kwa shekh yahaya nilitibiwa hapo kama upo dar es salaam
 
Ahsante,namshukuru mungu naendelea na matibabu,nimepata ahueni kidogo
 
Back
Top Bottom