Msaada wa kiafya: Kukohoa kikohozi kikavu mfululizo nitumie dawa gani ili nipone?

kjembe

Member
Jan 9, 2015
45
29
Wasalaam wadau naombeni ushauri, nina mdogo wangu wa kike yupo kidato cha nne sasa amekuwa akisumbuliwa na kikohozi kikavu(kisicho na makohozi) tangu mwezi february.

Baada ya kumpeleka hospitali walimpima vipimo kadhaa vikiwemo, minyoo, tyhpoid, malaria, full blood picture japo kuwa makohozi hayakuwepo hivyo hayakuchukuliwa
majibu yalionekana ana minyoo na upungufu wa damu kidogo, akapewa dawa za minyoo na ile syrup ya kuongeza damu.

Kifua kilitulia kwa muda wa wiki moja ya pili kikarudia tena, daktari akashauri aendeleze dawa za minyoo lakini bado kifua kinarudia juzi tu ameshauri achome sindano za allergy akisema pengine inaweza kuwa ni mzio(allergy).

Sasa wazazi wamekuwa na hofu kwa maana mtoto tangu azaliwe hana historia ya kifua na tiba anapewa lakini wapi.

Msaada wenu wana JF natumai mtanisaidia mawazo.
Natanguliza shukrani,
 
Atwange ama asage tangawizi bila kuchanganya na maji kama nusu kikombe cha chai then achanganye na asali mbichi halafu awe anakunywa vijiko vitatu kutwa mara tatu kama asipoona matokea mazuri baada ya wiki mbili basi aende kwa maspecialist hospitali kubwa
 
Atwange ama asage tangawizi bila kuchanganya na maji kama nusu kikombe cha chai then achanganye na asali mbichi halafu awe anakunywa vijiko vitatu kutwa mara tatu. Kama asipoona matokea mazuri baada ya wiki mbili basi aende kwa maspecialist hospitali kubwa
Shukrani mkuu
 
Naona wadau kama hili hawajalisema hapa,aka-check kifua kikuu pia maana vipeperushi vyao vinasema ukikohoa kikohozi kikavu zaidi ya wiki kadhaa inaweza kuwa dalili mojawapo.
 
Jaribu hii,choma magunzi ya mahindi,uchanganye na chumvi,uwe unalamba kutwa mara 3
au choma kokwa la parachichi mpaka liwe mkaa,then uwe unatumia unga wake
 
Jaribu hii,choma magunzi ya mahindi,uchanganye na chumvi,uwe unalamba kutwa mara 3
au choma kokwa la parachichi mpaka liwe mkaa,then uwe unatumia unga wake
Asante kwa ushauri, Hapo magunzi nichukue mangapi? i mean kipimo cha magunzi na pia cha chumvi.
Then, kwa unga wa kokwa la parachichi unatakiwa utumie vipi kwenye chai au arambe?
 
Sasa huyu ndugu yangu yeye kila kitu utafanyia kazi utamuoverdoze na kumletea complications ambazo hukutarajia afanye vipimo vya TB, HIV. Pia arudie doze ya minyoo aaangalie usafi wa chumba anacholala ama mazingira anayoshinda Je anatumia kuni kupikia n.k hivyo vyote vinaweza sababisha persistent coughing.
 
My first born was suffering similar to the explained symptoms then I went trough all kinds of treatment without success. Later unknowingly I decided to face an E.N.T. specialist ear, nose and throat where allergy was revealed and till now she is pretty fine. try this out ndugu.
 
Sasa huyu ndugu yangu yeye kila kitu utafanyia kazi utamuoverdoze na kumletea complications ambazo hukutarajia afanye vipimo vya TB, HIV. Pia arudie doze ya minyoo aaangalie usafi wa chumba anacholala ama mazingira anayoshinda Je anatumia kuni kupikia n.k hivyo vyote vinaweza sababisha persistent coughing.
TB, HIV pia hana.. Ndiyo maana nasema nitafanyia kazi baadhi ya ushauri uliopendekezwa
 
Jaribu hii,choma magunzi ya mahindi,uchanganye na chumvi,uwe unalamba kutwa mara 3
au choma kokwa la parachichi mpaka liwe mkaa,then uwe unatumia unga wake
Tafadhali naomba nielekeze vzr hii ya gunzi mi ni muathirika wa kikohozi kikavu pia
 
Back
Top Bottom