ZeMarcopolo
JF-Expert Member
- May 11, 2008
- 14,011
- 7,197
Leo nimesoma habari hii zoka Moshi.Mimi imenipa faraja kidogo lakini wasiwasi pia wa ukiukwaji wa haki za binaadamu kwa sababu kukamata mtu bila idhini yake na bila kibali toka kwenye vyombo vya sheria ni ukiukwaji wa haki za binaadamu.
wewe waonaje?
Halmashauri ya manispaa ya Moshi imeanzisha kampeni ya kudumu ya kuwakamata wagonjwa wa akili na kuwapatia matibabu katika hospitali ya Mawenzi mjini Moshi.
Kampeni hiyo imeanzishwa wakati wa wiki ya siku ya wauguzi duniani iliyokwenda sanjari na kupima afya za wanafunzi wa shule za msingi za kata ya Majengo katika manispaa hiyo.
Kaimu muuguzi mkuu wa manispaa ya Moshi Bi Anastazia Lyimo amesema kampeni hiyo ambayo hadi sasa imefanikiwa kwa kuwakamata wagonjwa wa akili watano, itawasaidia wagonjwa hao kuondokana na mateso wanayoyapata mitaani na jamii kuwa salama.
Amesema baada ya matibabu katika hospitali hiyo watapelekwa kituo cha wagonjwa wa akili cha Longuo ambako wanaendelea kupata matibabu na kutunzwa na baada ya wiki mbili au tatu wanakuwa katika hali nzuri.