Msaada wa jinsi ya kuunganisha Huawei modem kwenye Window 7

rmb

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
223
6
Heshima yenu wakuu!

Tafadhalini naomba kwa mwenye ufahamu anisaidie hili, nataka kuunganisha Huawei modem kwenye Laptop yangu, inatumia OS ya Window 7! Nimejaribu hii Modem kwenye Window XP inakubali haina shida,tatizo ni kwenye hii Window 7. Nikiinstall napata page inayosoma Mobile Partner kama kawaida na mtandao ninaotumia unakuja kama kawaida "EDGE Airtel TZ" na nimejaribu TiGo na VODA nao inasoma, tatizo sasa hapa kwenye Profile Name hakuna kinachotokea na nikijaribu kuconnect inagoma pia!

Nimejaribu kupiga kwa jamaa wa Customer Service wa Airtel wananiambia nikanunue Modem nyingine ya Airtel tu, na wakati nimewaambia hii hii Modem kwenye Window XP inafanya kazi, wameshindwa kunielekeza. Nadhani kuna setting sijazifanya kwenye hii kompyuta, na sijui naanzia wapi! Naomba anayejua asaidie katika hili
 
Rahisi sana kama tatizo ni 'Profile name' tu. Fanya hivi...

Tools --> Options --> Profile Management -->New. Hapa utatengeneza profile, unaweza kuipa jina lolote utakalo. APN ibaki static na ipe jina 'internet' access number mara nyingi *99# (actually hii itakuwepo pale otomatikli). Save, you are good to go
 
  • Thanks
Reactions: rmb
Mkuu Gurpta!
Nashkuru sana nimefanikiwa na sasa natumia modem yangu kwenye Win7 bila tatizo lolote! Tupo pamoja
 
Mimi pia nimefaidika JF ni ZAID ya mambo yote jamani.Hakuna kudanganyana hapa.
 
Back
Top Bottom