Hornet
JF-Expert Member
- Apr 29, 2013
- 26,117
- 49,473
Inawezekana ni kweli au siyo kweliGari ni kesi inayotembea....
Unanunuaje gari kwa mtu huendi kwenye vyombo husika kuhakikisha umiliki wake kama ni wa halali...? hata kama uneuziwa elfu 30...kwa nini usiende TRA na kwa Vehicle inspector kujua uhalali wa gari..?
Au ikute liliwahi kufanya matukio ya ujambazi, liligonga mtu akafa na mengineyo meengi...
Nina rafiki yangu alinunua Carina TI kwa mtu Dar akaja nayo Arusha, kaendesha wiki mbili tu wazee wa kazi wakampiga ngeta..
Kumbe gari liliwahi kufanya uhalifu mkoa fulani, likakimbiziwa Dar, Likauzwa Arusha...kesi ya gari ilikuwa ni mbaya sana
Wazee wa kazi walimpa kauli moja tu, "unaachia gari au tuondoke wote"
Jamaa akakubali yaishe, gari likaondoka na hakurudishiwa hata mia....Mmiliki halali akaenda kutafutwa akajibu mashtaka yake.....
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna kamchezo kanafanywa nowdays.