Msaada wa jinsi ya kubadili Kadi ya gari, aliyeniuzia naye alilinunua kwa mtu na hakubadili umiliki, Kadi bado inasoma aliyeliagiza nje

Ebale

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
940
1,000
Wakuu kama kichwa cha habari kinavyosema!

Nimenunua gari kwa mtu ambaye naye alilinunua kwa mtu na hakuwa amefanya mabadiliko ya kadi.

Nia yangu ni kuwa na kadi ya gari kwa jina langu. Kadi bado inasoma mmiliki wa kwanza. Nina document za mwanasheria za ununuzi.

Naomba msaada wa taratibu za kuwa na kadi kwenye hali hii.
 
tusipotoshane

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
733
1,000
Wakuu kama kichwa cha habari kinavyosema! nimenunua gari kwa mtu ambaye naye alilinunua kwa mtu na hakuwa amefanya mabadiliko ya kadi. Nia yangu ni kuwa na kadi ya gari kwa jina langu. Kadi bado inasoma mmiliki wa kwanza. NINA DOCUMENT ZA MWANASHERIA ZA UNUNUZI. Naomba msaada wa taratibu za kuwa na kadi kwenye hali hii.
Nenda TRA kitengo kinachoshughulikia usalama barabarani/leseni watakupa utaratibu wa kubadilisha,ni simple na fasta ukikamilisha taratibu.

Kila laheri kwa kumiliki gari,ni hatua katika maisha.Utakuwa rafiki wa visima vya mafuta na hardwares za akina Massawe.

Lipa Kodi kwa maendeleo ya nchi yako.

Sijakupotosha.
 
Ebale

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
940
1,000
Nenda TRA kitengo kinachoshughulikia usalama barabarani/leseni watakupa utaratibu wa kubadilisha,ni simple na fasta ukikamilisha taratibu.

Kila laheri kwa kumiliki gari,ni hatua katika maisha.Utakuwa rafiki wa visima vya mafuta na hardwares za akina Massawe.

Lipa Kodi kwa maendeleo ya nchi yako.

Sijakupotosha.
Shukrani sana kaka, ngoja nifanya hivyo
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,040
2,000
mtoa hoja bila shaka wachangiaji hapo juu wamekupa ushauri mzuri,ILA ndio matatizo ya kuishi ndani ya pithole country,magari yote ilitakiwa yaandikishwe kwenye local govt.(chini ya idara yao ya traffic)kwa hiyo gari inapochange hands ni wahusika kujaza form maalum(unazipata kwenye ofisi za serikali za mitaa) IDs za wahusika then mnunuzi unakwenda nazo kwenye civic center nz kubadilisha ownership(cha msingi hapa ni kufanya roadworthy na kupata traffic fine report ya gari husika,ili kuzuia madeni yaliyosababishwa na mmuzaji kuhamia kwako as mnunuzi)huu ndio utaraibu wa nchi zinazojielewa na sharia hizi tulikuwa nazo kabla ya huyu Tembo wetu anayeitwa TRA kuamua kubeba majukumu yote hadi driving licence upate kutoka kwao!!!
 
Boeing 747

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,779
2,000
Nenda TRA huko utajaza docs zao kisha utalipa 50000/- Hii inaitwa motor vehicle transfer fee....Hii unalipa wewe uliyeuziwa gari..

Aliyekuuzia atalipa 1% ya bei mliyouziana...Hii inaitwa stamp duty

Mkishakamilisha hayo, gari litakuwa lakwako kihalali na majina yako yatatokea kwenye card mpya na aliyekuuzia mkitoka nje, anakuomba lifti kwa heshima..

Please, usipuuze kukwepa hii 50000/- na hii 1%......imewatokea watu puani..
Nina ushahidi wa jamaa yangu hapa Arusha aliuziwa Carina Dar....kumbe ilikuwa magumashi na ilishasababisha ajali ikawa inasakwa na police kwa udi na uvumba...ilishikiwa Arusha...
Jamaa akaorodheshewa madhambi ile gari iliyofanya, akapewa options 2 tu....Unaachia gari au tupige kesi...
Jamaa akawa mpole akaachia gari....mpaka jana alikuwa anatembea kwa miguu..
Kwa sababu angepiga kesi, asingetoboa....mjasiriamali mwenye mtaji wa milioni 10 unapigaje kesi na serikali, kwa mfano..????
 
John7371

JF-Expert Member
Apr 29, 2018
1,007
2,000
Wakuu kama kichwa cha habari kinavyosema!

Nimenunua gari kwa mtu ambaye naye alilinunua kwa mtu na hakuwa amefanya mabadiliko ya kadi.

Nia yangu ni kuwa na kadi ya gari kwa jina langu. Kadi bado inasoma mmiliki wa kwanza. Nina document za mwanasheria za ununuzi.

Naomba msaada wa taratibu za kuwa na kadi kwenye hali hii.
Njia zipo tofuoti;
Firstly,mnunuzi wa kwanza aliyeuziwa gari ambaye ndiye aliyekuuzia wewe hope anao mkataba wa mauziano ya gari pamoja na kitambulisho cha original owner wa gari na kadi halisi pia wewe unayo;vikiwepo solving yake ni rahisi mno
 
John7371

JF-Expert Member
Apr 29, 2018
1,007
2,000
Secondly,Mwambie huyo aliyekuuzia akupe nakala ya mkataba ambao alipewa alipouziwa gari;uambatanishe na mkataba wa mauziano ambao alikupa wakati anakuuzia gari kisha mtafutie mwanasheria akuandikie mkataba mpya vizuri ambao utakusaidia kufanya transfer Kwa kushirikiana na first owner na second owner;kikubwa tu hapa ni kitambulisho cha mmiliki ambaye majina yake yanasomeka Kwenye kadi na Original card yenyewe. Please next time usinunue gari kabla ya kufanya kuthibitisha mmiliki halali wa gari manake ni rahisi kupewa card ambayo ilishakuwa transfered hivyo wewe upo na kadi useless
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,048
2,000
Kwan ukienda na mmiliki wa kwanza direct kisha mkajifanya ndo mnauziana moja kwa moja toka kwake kuja kwako kuna shida gani tena mnaandika mmeuziana kwa laki tano ili ile asilimia moja iwe ndogo
 
Munambefu

JF-Expert Member
Jun 24, 2012
1,382
2,000
Watu wengi hapo juu wamekueleza kwa lugha ya nyepesi na uongo kidogo.Nikuambie tu ukweli mkuu wewe ni mzembe kweli kweli!huwezi kuuziwa gari na mtu asiye mmiliki(aliyekuuzia bado hakuwa mmiliki),Pili hukwenda kuthibitisha usalama na uhalali wa hilo gari TRA,

tatu nikuhakikishie tu kwamba hutabadili kirahisi Kama walivyokushauri wengine.hiyo gari imeshakwepa transfer fee Mara moja,ukienda na mikataba hiyo miwili utalazimika kulipa zote mbili na penalty ya hiyo moja.
Huo Ndio ukweli japo unaumiza.
 
Alichodanganywa hapo ni kipi?Try to be specific
 
Boeing 747

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,779
2,000
Kwa lugha rahisi..kununua gari mkononi mwa mtanzania kama huna knowledge ya kutosha.., ni sawa na kucheza kamari..unaweza ukala au ukaliwa.........
 
John7371

JF-Expert Member
Apr 29, 2018
1,007
2,000
Kwa lugha rahisi..kununua gari mkononi mwa mtanzania kama huna knowledge ya kutosha.., ni sawa na kucheza kamari..unaweza ukala au ukaliwa.........
Siyo tu Bongo my friend;hata Japan usipokuwa makini na inspection reports na Mambo mengineyo you are dead and gone;I have a friend of mine alinunua Harrier old model from Japan through befoward and in two weeks hyo smoke yake na mlio wa engine acha tu;Its terrible!but the Car body was and it's still very very ok!That's why sometimes a very low price of the same car in the same auction should be a red flag to you!mfano ukiangalia walionunua magari befoward ambayo ni premium utayapenda best;yako Poa sana
 
And Still hapa bongo;kuna watu wanauza magari bora na magari problematic;Therefore tafuta fundi makini hata kama ni wa gharama usijalishe;asiwe tu ni just fundi otherwise you are finish! My first rule sikuzote kwenye maisha yangu-huwa simwamini dalali kwa maneno na sikuzote simpi nafasi ya ku ni manipulate akili yangu;na nikishaona hanipi nafasi ya ku judge mwenyewe hata kama kitu ni kizuri mno huwa sinunui tena;In school we were taught that sometimes advirtsement are misleading na hapo ndo matatizo yanapoanziaga;Hopeful kila mmoja she strategy yake binafsi anapokutana na madalali au wauza vitu
 
And fundi na dalali ukiwapa opportunity ya kulonga by experience you are finish;because they can collude
 
Lyamber

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
10,454
2,000
Siyo tu Bongo my friend;hata Japan usipokuwa makini na inspection reports na Mambo mengineyo you are dead and gone;I have a friend of mine alinunua Harrier old model from Japan through befoward and in two weeks hyo smoke yake na mlio wa engine acha tu;Its terrible!but the Car body was and it's still very very ok!That's why sometimes a very low price of the same car in the same auction should be a red flag to you!mfano ukiangalia walionunua magari befoward ambayo ni premium utayapenda best;yako Poa sana
Kampuni inayouza magari premium inaitwa japanesevehicles.com hao beforward wanasubiri..jamaa wanajiita trust company limites..
 
MANI

Platinum Member
Feb 22, 2010
7,287
2,000
Bila kitambulisho na picha ya mmiliki anaesoma kwenye kadi hii ngoma in ngumu itabidi afuate maagizo yako.
Secondly,Mwambie huyo aliyekuuzia akupe nakala ya mkataba ambao alipewa alipouziwa gari;uambatanishe na mkataba wa mauziano ambao alikupa wakati anakuuzia gari kisha mtafutie mwanasheria akuandikie mkataba mpya vizuri ambao utakusaidia kufanya transfer Kwa kushirikiana na first owner na second owner;kikubwa tu hapa ni kitambulisho cha mmiliki ambaye majina yake yanasomeka Kwenye kadi na Original card yenyewe. Please next time usinunue gari kabla ya kufanya kuthibitisha mmiliki halali wa gari manake ni rahisi kupewa card ambayo ilishakuwa transfered hivyo wewe upo na kadi useless
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom