Msaada wa huduma ya vinasaba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa huduma ya vinasaba

Discussion in 'JF Doctor' started by Haruna S, Mar 18, 2012.

 1. H

  Haruna S Member

  #1
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba mssada kama kuna mtu yoyote anajua kliniki hapa Tanzania wanaojishungulisha na kutoa huduma ya kupima vinasaba kati ya anayedhaniwa ni baba na mtoto?

  Na kama zipo matokeo yao niya uhakika?

  Na wanatoza kiasi gani?

  Nani muda gani inachukuwa mpaka kupewa matokeo?

  Shukrani!
   
 2. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,194
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Kwa huduma ya vinasaba, tafadhali endelea kusubiri wanaojua waje kukujuza. Ahsante kwa kuchagua jf jukwaa la JF DOCTORS!
   
 3. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,782
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  kupima DNA kunakwepeka....TUMIA CONDOMS KILA WAKATI.....
   
 4. mgeni10

  mgeni10 JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Dada Neema labda yeye anataka kujua kama alienae ndie Baba yake??????
  Na si kujua kama mtoto ni wake

  Hapo Condoms za nini?????
   
 5. k

  kisukari JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,482
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  jamani kiswahili kinatanuka.hili neno vinasaba,nilikuwa sijui kama ni DNA
   
 6. God knows

  God knows JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ukitaka kupima DNA ili kujua kama una mahusiano na mtu fulani, Nenda kwa Mkemia Mkuu wa Serikali. Kama upo Dar es Salaam, Ofisi yake inapatikana karibu na hospitali ya Ocean Road. Huduma hii hutolewa hapo ingawa sijajua gharama na procedure za kupatiwa huduma hii.
   
 7. H

  Haruna S Member

  #7
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kwa msaada
   
 8. H

  Haruna S Member

  #8
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru..nitafuatilia
   
 9. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ***
  Gharama ni laki moja kwa kila mmoja.
  Ila upimaji unafanywa kwa ombi la mahakama. Km kama kuna madai ya uthibitisho kwenye ugawaji wa mirathi.
  Ama kesi ya kukataa mtoto ambayo iko mahakamani.
   
 10. kvelia

  kvelia JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Muhimbili, Budando na pia hospital kubwa kama KCMC wantoa hiyo huduma. Wanaofanya kazi huko watujuze ni shs ngapi.
   
 11. H

  Haruna S Member

  #11
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimejaribu kufuatilia Muhimbili nimetoka kapa, hakuna aliyenipa maelezo ya uhakika labda kama kuna mtu anajua sehemu specific au mtu ambaye ninaweza kumuuliza.
   
 12. H

  Haruna S Member

  #12
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Laki moja ni gharama ya kuridhisha.Hakuna sehemu yoyote wanatoa hiyo huduma bila kupitia mahakamani
   
 13. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,643
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Mkuu uluza ofisi ya mkemia mkuu Wa serikali nadhani ni karibu na ocean road hospital unaweza saidika hapo
   
 14. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 4,928
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  kwenye lile zoezi la upimaji lilifanyika miaka ya nyuma kwa kila anayetaka kwenda iligundulika ASILIMIA 50 ya waliopimwa hawaendani na waliitwa ndo baba zao. Hivyo ikahofiwa kutatokea uvunjaji wa ndoa mkubwa na matukio ya kuuana kwa wanandoa kama imethibitishwa kuna cheating. Just imagine umesomesha watoto sita aafu unagundua mmoja tu ndo halali yako! Ikawekwa sheria ili wale watakaopimwa wewe kweli in claim ya kujua ukweli ndo maana lazima order itoke mahakamani sio kwa sababu tu umejisikia kupima. Wapo wanaochakachua si unajua tz si kila kilichopangwa ndo kinavyokuwa.
   
 15. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,149
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kweli tupo nyuma sana kimaendeleo
  DNA mpaka mahakama.
  Jesus Christ.
  OTIS
   
 16. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,643
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  mkuu ndo mahali pekee wanapoweza kufanya hiyo kipimo na tukujua wanaohitaji ni wengi wameona ili ku-limit the wahitaji then tuweke hiyo iwe na kibali cha mahakama, nadhani tukipata Musa wa kutuvusha jangwani salama kwenda nchi ya ahadi....uchumu wa kupaa, huduma bora za jamii, Afya, Elimu, Maji, n.k tunaweza kuwa na huduma ya vina saba kila hospitali ya mkoa na hata wilaya, mungu tusaidie
   
 17. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #17
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Yaani, hata mi nimeshangaa, hivi tutaendelea lini sisi?
   
Loading...