Msaada wa haraka wana jamvi la sheria Jumatatu nahitajika mahakamani

Nagweretu

Member
Jan 21, 2020
35
125
Yapata miezi kama kama miwili imepita Tangu nilipobomolewa mlango wa nyumba ya kupanga mida ya mchana na nikaibiwa vitu kadhaa ikiwepo TV , radio, pesa , vyombo na vitu vingine.

Wakati Tukio linafanyika nilikuwa kazini na wife nae alikuwa safari so nyumbani hapakubaki mtu. Baada ya tukio maisha mapya yakaendelea lakini nikawa napata taarifa kutoka kwa majirani kuwa anaeweza kufanya tukio Hilo hawezi kutoka mbali so ni Kati ya watu wanaonizunguka mmoja wao atakuwa amenifanyia wizi huo.

So moja kwa moja shutuma zikawa zinamuangukia mmoja Kati ya jirani yangu ambae Hana kazi yyte maalum halimi , sio mfanyabiashara , sio dalali wala kazi yoyote selikarini but ni mtu aneongoza kupiga Pampa ( kupendeza ) muda mwingi simu ipo sikioni na kuchart .

So eti amesikia kwa watu kuwa eti namshutumu kuwa yeye ndiye aliebomoa kwangu na kuniibia vitu

So wataalamu wa sheria kwanza hii ni Aina gani ya kesi?

J3 ninapoenda mahakamani nitegemee kupata mashitaka gani?

Je nikakubali kuwa yeye ni mwizi au Nikatae kuwa sikuwahi kusema maneno hayo , maana mtaa mzima wanamshutumu kwa tabia izo za wizi?

Nikienda mahakamani nikatoe hoja gani za kisheria kumaliza hii kesi mapema?

NATANGULIZA SHUKURANI ZA DHATI KWA MSAADA WOWOTE MTAKAONIPATIA WANAJANVI
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
37,262
2,000
Kuna umuhimu wa kila mtu kujifunza juu ya cross examination.Hata siku moja usiende mahakamani kama hujui kufanya au kufanyiwa cross examination.

Kana kuwa ulimwita mwizi ila omba mahakama umfanyie cross examination ili ajionyeshe mwenyewe kuwa yeye ni mwizi.

Nenda google jifunze juu ya cross examination ila kama umekuwa ukifuatilia kesi ya Mbowe basi utakuwa umejifunza mengi juu ya cross examination na utajishukuru wewe mwenyewe kwa kufanya hilo.

Lakini ni muhimu utafute mwanasheria kwani mahakamani ni sawa na kwenda hospitali,huwezi kujitibu mwenyewe bila ya dokta.Na mahakamani ni hivyo hivyo,huwezi kujitetea mwenyewe bila mwanasheria.
 
aise

JF-Expert Member
May 16, 2018
2,873
2,000
Yaani umeibiwa,
halafu umefunguliwa kesi.

na kwa mujibu wa maelezo yako hapo juu inaonekana unaogopa kwelikweli.

Na huenda jela ikakuhusu kwa woga huo.

Nielekeze gereza la karibu yako niwe nakuletea walau sabuni.
 
Ghiti Milimo

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
3,178
2,000
Yaani umeibiwa,
halafu umefunguliwa kesi.

na kwa mujibu wa maelezo yako hapo juu inaonekana unaogopa kwelikweli.

Na huenda jela ikakuhusu kwa woga huo.

Nielekeze gereza la karibu yako niwe nakuletea walau sabuni.
Mmmmmmmm! JF imeingiliwa! Huo ndiyo ushauri wako? Au wewe ndiye huyo MTUHUMIWA?
 
Nagweretu

Member
Jan 21, 2020
35
125
wewe kataa hukusema mkuu.....kwani kuna aliekurecord sauti ukishutumu? Kama hayupo wewe komaa nae kuwa aoneshe ushahidi wa video au sauti yako ikimshutumu na kama anaitwa said umuulize dunia hii kuna kina said wangapi, kwahiyo nisitaje jina said kwasababu yako
Hakuna alierecord
 
Nagweretu

Member
Jan 21, 2020
35
125
Kuna umuhimu wa kila mtu kujifunza juu ya cross examination.Hata siku moja usiende mahakamani kama hujui kufanya au kufanyiwa cross examination.

Kana kuwa ulimwita mwizi ila omba mahakama umfanyie cross examination ili ajionyeshe mwenyewe kuwa yeye ni mwizi.

Nenda google jifunze juu ya cross examination ila kama umekuwa ukifuatilia kesi ya Mbowe basi utakuwa umejifunza mengi juu ya cross examination na utajishukuru wewe mwenyewe kwa kufanya hilo.

Lakini ni muhimu utafute mwanasheria kwani mahakamani ni sawa na kwenda hospitali,huwezi kujitibu mwenyewe bila ya dokta.Na mahakamani ni hivyo hivyo,huwezi kujitetea mwenyewe bila mwanasheria.
Nitaufanyia kazi ushaur wako
 
Nagweretu

Member
Jan 21, 2020
35
125
Yaani umeibiwa,
halafu umefunguliwa kesi.

na kwa mujibu wa maelezo yako hapo juu inaonekana unaogopa kwelikweli.

Na huenda jela ikakuhusu kwa woga huo.

Nielekeze gereza la karibu yako niwe nakuletea walau sabuni.
Mazimbu moro
 
chapangombe

Senior Member
Sep 28, 2014
197
250
Yapata miezi kama kama miwili imepita Tangu nilipobomolewa mlango wa nyumba ya kupanga mida ya mchana na nikaibiwa vitu kadhaa ikiwepo TV , radio, pesa , vyombo na vitu vingine.

Wakati Tukio linafanyika nilikuwa kazini na wife nae alikuwa safari so nyumbani hapakubaki mtu. Baada ya tukio maisha mapya yakaendelea lakini nikawa napata taarifa kutoka kwa majirani kuwa anaeweza kufanya tukio Hilo hawezi kutoka mbali so ni Kati ya watu wanaonizunguka mmoja wao atakuwa amenifanyia wizi huo.

So moja kwa moja shutuma zikawa zinamuangukia mmoja Kati ya jirani yangu ambae Hana kazi yyte maalum halimi , sio mfanyabiashara , sio dalali wala kazi yoyote selikarini but ni mtu aneongoza kupiga Pampa ( kupendeza ) muda mwingi simu ipo sikioni na kuchart .

So eti amesikia kwa watu kuwa eti namshutumu kuwa yeye ndiye aliebomoa kwangu na kuniibia vitu

So wataalamu wa sheria kwanza hii ni Aina gani ya kesi?

J3 ninapoenda mahakamani nitegemee kupata mashitaka gani?

Je nikakubali kuwa yeye ni mwizi au Nikatae kuwa sikuwahi kusema maneno hayo , maana mtaa mzima wanamshutumu kwa tabia izo za wizi?

Nikienda mahakamani nikatoe hoja gani za kisheria kumaliza hii kesi mapema?

NATANGULIZA SHUKURANI ZA DHATI KWA MSAADA WOWOTE MTAKAONIPATIA WANAJANVI
Huyo amekufungulia kesi ya defamation ipo katika Tort laws ( kumdhalilisha) hiyo unamnyuka mapema tu!
 
Nagweretu

Member
Jan 21, 2020
35
125
Poleni na majukumu wanajanvi nashukuruni Sana Kwa kunipa mawazo chanya juu ya kesi niliyowaambia inanikabili,
Sijawapa update juu ya nini kilifanyika mahakamani j3 siku niliyoitwa Kwa wito.
Kiufupi ni kwamba J3 sikuhudhuria mahakamani kwa kukataa kuwa wito nilioletewa sio wangu kwani majina Sio yangu , wito nilioletewa ulikuwa na majina mawili la kwanza Baba mzazi na pili lilikuwa la babu but na jina la babu nalo lilikosewa herufi moja na jina la kwanza halikuandikwa , baada ya siku kama tatu nikachomoka kuelekea rikizo ya mwezi mmoja Ivo , so nataka nikutane nae January nikapambane Naye vizur
 
Mc cane

JF-Expert Member
May 18, 2018
5,496
2,000
Ukiitwa Mahakamani, ule wito huwa una ainisha kosa lililofanya ushtakiwe, sasa sijui wewe unaenda mahakamani basing on what

Pili, Mahakamani kataa kwamba hukumshtumu (kama itakuwa kesi ya Defamation/kashfa)

Mwisho nakushauri nenda karipoti hilo tukio la wizi polisi

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom