Msaada wa haraka wa tiba, Mtarajiwa wangu ana umbo nene sana

themanhimself176

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,803
2,825
Ni siku nyingine tena wadau wa MMU inayopendeza machoni mwetu shukrani pekee kwa Allah swalie tumefikisha mpk leo hii tupo hai na tunapumua bure hii sio kwa uwezo wetu bali kwa neema zake pekee kwa uchache kabisa tushukuru kwake yeye alie katika kiti cha enzi

Pili kwa waislamu wenzangu niwatakie mfungo mwema wa ramadan hakika huu ndo mwezi wa toba na Allah atujalie tuwe miongoni mwa tutakao nufaika na mwezi Amin
Basi ngoja niende moja kwa moja kwa maudhui ya huu uzi

Wadau niko na mwenzangu ambae ndo natarajia Inn Shaa Allah awe kuwa mama watoto wangu ila tatizo uyo mwenzangu mwili wake, yuko na umbo kubwa kuliko maelezo inshort ni mnene saaaaaana na hasa tumbo ni kubwa kiliko maelezo na mwenzangu yuko na asili ya asia hawa watu wa udongo wa dubai sasa vuta picha

Mavazi yake ni stara maashaallah na ameshika dini vizuri na ndo miongoni mwa vitu ambavyo vinanifanya nijiweke pale maana ana msingi mzuri wa dini. Basi wadau nisiwachoshi na swaum hii nilikuwa nahitaji msaada wa tiba yoyote ile ya kupunguza mwili mana yuko na miaka 24 lakini ni kama mmama mwenye miaka 30 labda na watoto 3 au wa 4 wa haraka haraka

Na kibaya ni kwamba naona kama mama anataka kuleta maneno mana kila siku na mwambia mama mkwe wako ni flani na anamfaham uzuri tu ila anakataa kisa mwili eti atuendani mana mie kimwili changu kidg na nikiwa nae ni kama mtu na mama yake.

Ili kuondoa hii kadhaa nahitaji kufahamishwa tiba tuu na sio lingine labda na maujanja mengine kama yapo
Nawasilisha
 
azunguke uwanja mara 20 kwa siku

push-up 200 kwa siku..

mazoezi ya kuruka vihunzi na visiki..
yaan kiufup apige mazoez ya aina zote

baada ya hapo anywe maji ya moto yaliyochanganywa na malimao lita 8 kwa siku... namaanisha anywe maji ya vuguvugu ya kutosha..

afanye dayati.. ale embe tu kwa siku ..

asipopungua ndan ya mwaka mmoja bhas ana lake jambo
 
Asubuhi na jioni awe anafanya mazoezi.
Inabidi yeye mwenyewe akubali kufanya mazoezi la sivyo mazoezi kwake itakuwa kama mateso.
Nia tu atapunguza vizuri tu huo mwili.
Pamoja na diet.
 
Mwambie afanye diet na afanye mazoezi kwa sana itamsaidia na pia aepuke kula vyakula vyenye mafuta mengi
 
Mkuu;
Unampenda kweli au unamtania mtoto wa watu?? Kumbuka, kama utawasikiliza watu kuhusu unayemtaka awe mkeo, hutampata hata mmoja wa kukufaa. Jiulize, si ni weye ulimtongoza huyu binti?? Ulipomwona na kuamua kumpa fasihi zako, si alikuwa na mwili huo huo?? Kipenda roho hula nyama mbichi. Hizo ndo nyama mbichi mkuu. Ukubwa wa mwili ndio uliutaka sio kimbaombao. Hivyo vipo ila si cha kutengeneza, sasa huu mbuyu wako unataka ufanane na mnazi si unataka kumuua mtoto wa watu??
Mkatae wenzio wachukua kama lilivyo kama hutajinyonga kwa wivu siku utamkuta na mitoto yake 4 na weye na kimbaombao chako huna mtoto.
Mrembo ni machoni kwako mkuu si kwa mwingine.
 
Mkuu;
Unampenda kweli au unamtania mtoto wa watu?? Kumbuka, kama utawasikiliza watu kuhusu unayemtaka awe mkeo, hutampata hata mmoja wa kukufaa. Jiulize, si ni weye ulimtongoza huyu binti?? Ulipomwona na kuamua kumpa fasihi zako, si alikuwa na mwili huo huo?? Kipenda roho hula nyama mbichi. Hizo ndo nyama mbichi mkuu. Ukubwa wa mwili ndio uliutaka sio kimbaombao. Hivyo vipo ila si cha kutengeneza, sasa huu mbuyu wako unataka ufanane na mnazi si unataka kumuua mtoto wa watu??
Mkatae wenzio wachukua kama lilivyo kama hutajinyonga kwa wivu siku utamkuta na mitoto yake 4 na weye na kimbaombao chako huna mtoto.
Mrembo ni machoni kwako mkuu si kwa mwingine.

Duuuuh umetisha mkuu

Ila trust me i do love her

Ila ni mwili mkuu ana mwili mkubwa na ndomana nikaomba ushauri wa namna atakavyo punguza mwili ila sio kumwacha mana ndo first grl wangu since niko p6 i used to be with her
 
hakuna kiumbe kilicho static,wote tupo dynamic...tena in all aspects iwe financially,kimwili,kimazingira etc....kama unampenda utamuoa tu regardless ya mwili wake ila kama ulimpendea mwili basi utamtosa....halafu bora tu ufungulie ka umefunga naona unakaa njaa tu....
 
Kama ni tiba waone mawakala wa forever living! Wana products za kupunguza unene kwa wale wavivu wa mazoezi!!! Andaa almost laki tatu.... Kama huna hela basi atumie njia ya kawaida... Diet na mazoezi

Huwezi mlazimisha mtu apungue... Inabidi yeye mwenyewe aamue kupungua. La sivyo mtadanganyana tu! Ishu ya kupungua si mchezo ati!!!
 
Back
Top Bottom