Msaada wa haraka tafadhali kuku wangu hawatagi kabisa

Aug 2, 2011
50
55
Habari wadau!

Ninatatizo kubwa sana katika hizi harakati za kujikwamua kiuchumi, mimi ni mfugaji wa kuku wa kisasa wa mayai (Layers) tangu waanze kutaga huu ni mwezi wa 4 sasa, lakini utagaji wake umekuwa wa kusuasua sana toka waanze kutaga.

Cha ajabu zaidi sasa hivi wanataga tray 5 tu kwa siku kati ya kuku 1020. Nilikuwa nanunua chakula kampuni moja inaitwa Multivate farm Ltd ambayo ndo inaleta huku kusini vyakula vya kuku lakini utagaji wa kuku wangu ukawa bado mdogo. Nikaamua kutengeneza mwenyewe chakula lakini mambo bado ni yaleyale tu hakuna madadiliko yoyote niliyoyapata, naombeni msaada nifanyeje ili kuku wangu warudi kwenye hali yake ya utagaji na waweze kutaga vizuri.

Nawasilisha kwa msaada zaidi

Asanteni
 
1. Je ulifanya ukaguzu kuwatenga wanao taga na wasio taga? Make huwa kuna tasa kabisa.

2. Ratio ya chakula ikoje? Wanakula wanatosheka? Au una wa Over feed? Au
una wa Under feed?

3. Mazingira yao yakoje hasa banda je kuna utulivu wa kutosha au wana tishwa tishwa na wanyama kama paka?

4.Je hawali mayai? Kwamba wakitaga wana yala mayai.

5. Je una simamia mwenyewe? Vijana hawaibi mayai?

6. Una uhakika na chakula ulicho jitengenezea? Ulienda kukipima kujua kuna DCP kiasi gani? Yaani Digestive Crude Protein.

7. Hao kuku ulinunu pure kutoka kwenye kampuni inayo aminika na kutambulika?

8. Hawakuwahi kuugua? Hawaumwi? Hawana aina yoyote ya ugonjwa?


Kati ya hayo hapo aababu iko humo humo.
 
1. Je ulifanya ukaguzu kuwatenga wanao taga na wasio taga? Make huwa kuna tasa kabisa.

2. Ratio ya chakula ikoje? Wanakula wanatosheka? Au una wa Over feed? Au
una wa Under feed?

3. Mazingira yao yakoje hasa banda je kuna utulivu wa kutosha au wana tishwa tishwa na wanyama kama paka?

4.Je hawali mayai? Kwamba wakitaga wana yala mayai...
Asante kwa mchango wako mkuu,ila kuhusu mambo uliyosema ni kama hifatavyo, kuhusu banda liko vizuri,kuhusu wanyama hakuna zaidi ya ndege wakipita mda mwingine ndo wanapiga kelele na panya usiku mda mwingine ndo wanawazingua,chakula natumia damu, Mifupa, chokaa, dagaa, mashudu ya alizeti, pumba, mahindi na Primix kuchanganya,pia vijana wangu hawaiiibi,mwanzo walivyoanza kutaga walienda mpaka tray 24 per day.

then ndo wakaanza kudrop kila siku, ndo mpaka leo ndo matokeo hayo,kuku wako kwenye cage,wachache ndo wako chini, in case yai likipasuka wanakula na wa chini wanadonoana ila huwa nawawekea majani, kuhusu kuumwa hawaumwi na chanjo zote walipata,ratio ya chakula nawapa 130grms per chick per day.usafi ndani ya banda unafanyika 2X per week.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom