Dogo G
JF-Expert Member
- Jul 6, 2018
- 1,052
- 440
Isee ni hatari sana.Inahuzunisha sio kidogo saaaana,nimeingiwa na huruma ghafla.Katika kupitapita youtube kujua yaliyojiri nimekutana na clip moja iliyorushwa na online tv moja nimeshindwa kuiweka hapa.Katika hiyo clip kuna mwanajeshi wa kenya anaomba msaada toka kwa serikali ya nchi yake kutokana na kuwa mateka kule somalia.
Huyo mwanajeshi ameonekana anazungumza kwa hofu akitetemeka huku akijitambulisha jina lake,nyumbani anakotokea(jina la mtaa na mji),namba ya kikosi anachotoka na taarifa nyingine nyingi kutoka katika jeshi la kenya KDF.Mwanajeshi huyu amedai hayuko peke yake bali ametekwa na wenzie wengine wasiopungua 20 ambapo wanauawa taratibu kutokana na kuchelewa kwa msaada toka kwa serikali.
Ikimbukwe tu hawa wanajeshi wa kenya walitumwa kule somalia kwaajili ya kulinda amani inayochafuliwa na vikundi vya waasi ikiwemo al-shaabab.Kiongozi wa alshaabab aliwahi kuhojiwa akasema madhila wanayoyafanya kenya kila siku hayataisha mpaka pale serikali ya kenya itakapowaondoa wanajeshi wake kule somalia,na wataendelea kuwaangamiza wanajeshi wa KDF siku zote.
Sasa wakuu sijaelewa ni kwanini raisi wa kenya anashindwa kutoa kauli wakati wanajeshi wametekwa wana miezi zaidi ya mitano.Kenya chukueni hatua kwa walinzi wa taifa.Ni lazma muangalie risk itakayozidi kujitokeza iwapo hawo wanajeshi wataendelea kubaki mikononi mwa alshaabab mfano watakuwa wanatoa siri za KDF ili wasiteswe zaidi.
Source:2020 tv/online tv
Sent using Jamii Forums mobile app