Msaada wa haraka: Nakaribia kufungwa

Fadhili Paulo

JF-Expert Member
Sep 1, 2011
3,211
988
Habari zenu Wakuu,


Kuna rafiki yangu alinikopa laki 3 tarehe 1 mwezi November mwaka huu, tukaandikishana na kutiliana saini mimi, yeye na rafiki mwingine kama mdhamini kwani ndiye aliyenitambulisha kwa huyu rafiki mkopeshaji, katika saini hizo mkopeshaji alinitaka nimrudhie laki nne na nusu tarehe 30 Novemba yaani jana, kwa bahati mbaya mpaka jana nimeshindwa kupata hiyo laki nne na nusu bali nimempelekea laki 2 amekataa anadai nimekiuka makubaliano na kuwa kama naendelea kuchelewesha mwezi mwingine nitakuja kulipa laki na nusu zaidi yaani sasa mpaka tarehe 31 Desemba nitatakiwa kulipa laki 6 lasivyo ananifunga.


Msaada wenu jamani nitamtokaje hakimu hapa? kwani ninauhakika mpaka muda huo sina uhakika kama nitakuwa nimepata.


Msaada wenu wa mawazo jamani.
 
Dawa ya Deni ni kulipa. Ushauri sasa, hivyo nivitisho tuu Deni huwa halimfungi mtu. Maadamu umeonyesha niya kulipa na hataki kupokea hela zake basi muache akufunge tuone. Lasivyo mabenki yangefunga wengi. Cha msingi hakikisha unaweka ushahidi kuwa ulimpelekea nusu yake, na ukamuomba ummalizie nyingine Kwa kipindi mtakacho kubaliana akakataa pia.

Ila Kwa kutengeneza mahusiano kama unayo hiyo pesa mlipe. Lakini kukutisha na kifungo si kweli kaka.
 
Kakope sehemu ingine umlipe kuepuka mlundikano wa riba (lipa deni kwa kutumia deni jipya)

Ushauri hapo juu ndio haswa sahihi na ndio tunavyoishi hapa mjini. Hata kwenye mabenki unakopa huku, wakijitokeza wengine wenye riba na masharti nafuu unaenda chukua huko unalipa huku nyingine unaendelea kusongesha maisha mjini.

Cha msingi hapo usikope bila kuwa na uhakika wa kurudisha ingawa "mpango si Matumizi" unaweza kopa ukiwa na malengo thabiti lakini lolote linaweza kutokea usifikie malengo.

Hakikisha unakopa kiasi ambacho unauwezo nacho kulipa taratibu kulingana na kipato chako. Kiasi cha kulipia deni kisizidi 40% ya "gross profit" ili usije dhalilishwa hapa mjini endapo mambo yataenda mrama kama yaliyokukuta.
 
Kweli kakope kwingine Laki mbili na nusu jazia na hiyo laki mbili mpelekee 450,000/= hao watu sio wazuri maana akiikamata hiyo hela atakata riba 150,000/= akuache na 50,000/=
Hata mahakamani utapewa muda kama unazo kidogo lakini ukigoma kumlipa hata senti siku hizi wanawekwa jela na kulipiwa malazi na chakula ukitoka unalipa vyote deni na chakula/ malazi uliyoyatumikia
Mpelekee 450,000/= mbele ya Mdhamini au shahidi au Balozi
 
Riba ya 50% kwa mwezi? Huu ni wizi wa mchana! Huyo jamaa ndio biashara yake? Ana leseni ya kufanya hiyo bishara?
Ndiyo mkuu ndiyo biashara yake ila hana leseni na hata kama angekuwa na leseni sidhani kama angeruhusiwa na vyombo husika.
 
Kakope sehemu ingine umlipe kuepuka mlundikano wa riba (lipa deni kwa kutumia deni jipya)
Mkuu, nashukuru kwa ushauri wako ila suala la kwenda kukopa kwingine hilo ndilo gumu sitaki kabisa kusikia tena mambo kama haya ni bora anipeleke polisi.
 
Kweli kakope kwingine Laki mbili na nusu jazia na hiyo laki mbili mpelekee 450,000/= hao watu sio wazuri maana akiikamata hiyo hela atakata riba 150,000/= akuache na 50,000/=
Hata mahakamani utapewa muda kama unazo kidogo lakini ukigoma kumlipa hata senti siku hizi wanawekwa jela na kulipiwa malazi na chakula ukitoka unalipa vyote deni na chakula/ malazi uliyoyatumikia
Mpelekee 450,000/= mbele ya Mdhamini au shahidi au Balozi

Hapana mkuu sipo tayari kuongeza pressure zingine, hiyo laki 2 aliyokataa ninayo na siwezi kumwachia bila kuandikishana, nipo tayari kwenda jela sema nitaimiss sana jf.
 
Fadhili, usipate hofu. Mkataba mliofunga ni wa kukopeshana na kukiuka masharti ya deni haiwezi kufanya mtu aliyeshindwa kulilipa kufungwa. Kama bado anaendelea kukataa hela ulizonazo pamoja na kuwa wewe unampa basi zitunze utampa siku atakayofungua kesi.

Kumbuka kuwa kisheria haitakiwi Malipo ya deni na. riba kuzidi kiasi kilichokopwa. Hii inaitwa duplum principle. Wale mashylocke wanaoishi kwa riba za mikopo hawataipenda hii lakini that's the fact.
 
Kumbuka kuwa kisheria haitakiwi Malipo ya deni na. riba kuzidi kiasi kilichokopwa. Hii inaitwa duplum principle. Wale mashylocke wanaoishi kwa riba za mikopo hawataipenda hii lakini that's the fact.

Hapa sijakuelewa. Unaweza kutoa mfano..?
 
Hawezi kukufunga kwa civil case!labda awe anakulipia gharama zote za jela ambazo zitakua ni zaidi ya hilo deni!by the way mtu anayefanya biashara ya riba lazima awe na kibali cha BOT na sio kufanya tuu kwasababu atakua anakwepa kodi.for what I know hapo hakuna kesi ya kufungwa.
 
Machakato mgumu sana ndugu yangu
maisha haya yaleta ugumu sana pasipo kutarajia , jipe nguvu ya utambuzi , lakini kwa hili huna haja ya kusikitika.
Kwa kuleta ushahidi zaidi Nenda kwake na simu ya audio rec. ongea kwa Msisitizo ukimuomba apokee hicho ulicho nacho.
pia wa weza andika barua ya ombi la kukuvumialia kwa kipindi hiki ili umlipe.
Nakuomba uepuke sana watu wa aina hii, maana sio wastaarabu hata kidogo wako na roho kutu
 
Back
Top Bottom