msaada wa haraka.mwili kukakamaa na kupoteza fahamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

msaada wa haraka.mwili kukakamaa na kupoteza fahamu

Discussion in 'JF Doctor' started by T2015CCM, Oct 5, 2012.

 1. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  salaam wana jf.

  naombeni msaada wa haraka.

  kuna ndugu yangu anakusa pumzi,unakuta anaanza kukoroma kama mtu aliebanwa koo, then analegea mwili wake baada ya muda unamuona anakakamaa anajinyosha as if mtu anapoteza roho.baadae anapoteza fahamu anakuwa hajitambui.

  anakuwa hawezi kupumua hadi umpepee.akizinduka anakuwa nakiu kali kubwa ya maji.ukimuuliza kilichotokea hajui hata kidogo anakushangaa unachomuuliza.

  je hili ni tatizo gani???

  dawa yake ni nini??? siku zote za maisha yake hajawahi kuwa kuwa na tatizo hili,limeanza kama wiki moja sasa.
   
 2. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Pole mpeleke haraka hospitali akapate vipimo ijulikane wazi kwanza anaumwa nini ndipo urudi hapa haraka. Nitajie uzito wake, urefu wake na jinsia yake.
   
 3. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  asante kwa ushauri.ana uzito wa kg 60, ni mwanamke na ni mfupi sina uhakika ni sm ngp bt ni mfupi
   
 4. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Okay, mpeleke hospitali kwa vipimo. Lakini kwa sasa wakati akijiandaa kwenda hospitali mwambie asinywe chai ya rangi, kahawa, soda yeyote, kilevi chochote, asivute chochote na asile chakula kigumu kinachohitaji maji mengi ili kumeng'enywa na umpe maji glasi 1 kila baada ya masaa 2. Akishapima urudi.
   
 5. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  au sukari inashuka
   
 6. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  asante kiongozi.umesema akipima nirudi hapa au wapi.
   
 7. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Urudi hapa jukwaani mkuu, ikishajulikana anasumbuliwa na ugonjwa gani hasa ndo wanajukwaa watakueleza namna gani afanye ili apone na pengine namna gani aishi ili siku nyingine asipatwe na tatizo hilo tena. Usichelewe.
   
 8. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kuna uwezekano labda ni majini mpeleke akaombewe maana unaweza ukakuta ni mchezo wa wadunia. kuna dada yangu alikuwa natatizo hilo tulienda hospital hatukuweza fanikiwa ala tulipompelekea kwenye maombi naona amefanikiwa siku hizi mzima
   
 9. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Pole sana mjielekeze na kwenye maombi
   
 10. D

  Diga Diga Senior Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ID yako tu inatosha kukuelezea wewe ni mtu wa namna gani! Unaomba msaada hapa JF kwa mtu mgonjwa kweli? Hivi uko serious kweli wewe? Hujui hospitali zilipo? Muda wa ku-post hapa unautoa wapi badala ya kumuwahisha mgonjwa hospitali? Wiki sasa imepita, wewe leo ndio unaomba msaada! Ama kweli wewe ni Rais wa Migomo, umegoma kumpeleka mgonjwa hospitali badala yake umekubali kung'ang'ana na keyboard ili uombe ushauri JF. Ungekuwa umeshampeleka mgonjwa hospitali kwanza, akapimwa na kupewa ushauri wa kitaalam, mkatimiza maelekezo ya daktari kwa ufasaha lakini bila mabadiliko ya hali ya mgonjwa hapo ungekuwa wa maana sana kuja kuomba ushauri hapa. Ila wewe umeuguliwa kwa wiki nzima, ukakaa kimya (as if you are in comma) ila ulipozinduka ukaja ku-post uzi hapa jukwaani! What a nonsense!
   
 11. k

  kim jong un JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  aende hospitali hujasema umri lakin kilo 60 ni mtu mzima kidogo kama imetokea zaidi ya mara tatu nadani ya miezi sita hiyo itakuwa ni epilepsy yaan kifafa,

  jambo ambalo si kawaida kuanza ukubwani LAKINI inawezekana alikuwa nacho lakin kinaongezeka kidogo kidogo.......... au alipata ajali zikamuumiza kichwani, au kuna dawa anatumia ambazo zinaweza kuleta kifafa, drug induced epilepsy also madawa ya kulevya, au ANA UVIMBE KWENYE UBONGO

  other wise anashinda njaa sana anapata hypoglycaemia au kama ana kisukari anaweza kuwa anapata DKA AU HHS

  afanye EEG na CT scan pole
   
Loading...