Msaada wa haraka kwa tatizo la jino tafadhali

Amri kuu ni Upendo

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
789
474
Mwaka 2003 gego langu la mwishoni juu kushoto lilianza kutoboka taratibu na kuuma. Mpaka 2008 likawa limetoboka kabisa na kuanza maumivu makali.Watu kadhaa wamenishauri nisiling'oe eti laweza kuniletea matatizo makubwa katika ung'oaji wake. Mganga mmoja aliwahi kunipa dawa ya kienyeji ambayo ilifuta kabisa maumivu ya jino tangu 2008 hadi mwaka jana, lakini mwaka huu tena maumivu yamerudi yakiambatana na kuvimba kwa fizi. Sasa natamani kuling'oa jino hili ila naomba madaktari wataalamu wa meno wanishauri na ikiwezekana ni kwa namna gani ung'oaji wa jino hili unaweza kufanyika kwa usalama na wapi kwa hapa Dsm naweza kumpata daktari bingwa wa meno. ASANTENI
 
Nyuma ya lilipokua jengo la umoja wa vijana-ccm, wapo kati ya mzizima na zanaki. Wanatazamana na jela ya watoto. Nimesahau jina la mtaa ni kama makutano ya fire na allykhan.

Mia Mkuu, hii Regency hospital ipo wapi hapa Dar? Naomba nielekeze.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom