Msaada wa haraka kwa Mtanzania aliyezidiwa hospitali Urusi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa haraka kwa Mtanzania aliyezidiwa hospitali Urusi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nderingosha, Mar 22, 2011.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana jamii,najua hapa inaweza kuwa sio mahali pake lakini naomba nitumie jukwaa hili kuleta kwenu habari ya kusikitisha sana na inayohitaji suluhisho la haraka sana kutoka serikali ya Tanzania.Nimepokea taarifa za uhakika toka kwa jamaa urusi anayesema kwamba kule urusi kuna mtanzania anaitwa Justin(ni muhaya-sikui jina la baba yake)ambaye alikuwa anasumbuliwa na tatizo la shinikizo kubwa la damu(hypertension)kwa muda mrefu pasipo kutumia dawa(alishauriwa atumie akazembea).Huyu kijana taarifa ni kwamba kwa siku sita sasa yuko kwanye coma(amepoteza fahamu)baada ya kupata kiharusi(stroke) na amelazwa hospitali taabani akiwa pia ame paralyze mwili mzima.Hali yake ni taabani na madaktari wamesema hawatamfanyia operation kwa kuwa prognosis(matokeo hayatakuwa mazuri)kwani anaweza kupoteza maisha kutokana na damu kumwagika ubongoni.Kinachosikitisha sana ni kwamba hakuna wa kumsaidia kwani:

  • Hakuwa na registration ya kuishi nchini urusi(si mwanafunzi)
  • Hana ndugu urusi(watanzania wanaomfahamu-wahaya wenzake) wamemtelekeza
  • Ubalozi umesema hawawezi kumsaidia
  • Hospitali zinatakiwa zilipwe hela za kumhudumia(ni gharama kubwa hospitali-karibu dola 75 kwa siku)
  • Ndugu zake Tanzania yaelekea nao wamemtelekeza
  • Ambaye ametuma ujumbe huu(mwanafunzi)amejaribu awezavyo kutafuta ndugu zake Tanzania kwa simu lakini wanaonekana kutojali
  • Hamna wa kukaa nae hospital kumhudumia kwani hajitambui
  Kinachotakiwa: Kama kuna mtu yoyote anayeweza kufikisha habari hizi hata wizara ya mambo ya nje hapa Tanzania,tafadhali hima hima kwani njia iliyobaki ni kumsaidia huyu bwana arusishwe Tanzania haraka asifie urusi.Wenye contact zozote na watu wanaoweza kusaidia wafanye hima jamani.Mi nimeleta ujumbe hapa jukwaani kwani hiki ndicho nachoweza kufanya kwa nafasi yangu.Shukrani
   
 2. luckyperc

  luckyperc JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa haraka*2 ungefungua mtandao wa wizara ya mambo ya nje, ukatuma kwenye email yao.
  I think z better.
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,325
  Trophy Points: 280
  nderingosha,
  kwanza pole kwa hali ya huyo Mtanzania mwenzetu huko Ughaibuni,
  Pili asante kwa kuonyesha concern.
  Kwa hali uliyoieleza, kama yuko kwenye comma, that means yuko ICU hakuja jinsi yoyote ya kumsafirisha mtu on ICU, unless kupitia flying doctors na ndege zao za kukodi, kwa long distance kama huko, it simply doesn't work.
  Kwa vile hata surname yake hujaipata, fanya bnidii kuipata, ili angalau ikijulikana, watu wa karibu wanaweza just tyo show concern hata kama there is nothing much they can do.
  Mimi concern yangu ni Ubalozi wetu huko kutojali eti kwa sababu hana status!. Huo ubalozi unafanya nini?.

  Naomba niwape ushuhuda jinsi balozi za wenzetui, zinavyothamini raia wake, nikitolea mfano Ubalozi wa Uingereza jijini Dar es Salaam. Kukitokea raia yoyote wa Uingereza, amepata tatizo lolote, Ubalozi utatuma ofisa wake physically kwenda kumuona na kujua mahitaji yake ni nini, just to show concern.

  Mwaka jana , jamaa mmoja ambaye ni mzungu wa unga wa Ilala, amekamatwa airport akijaribu kupandisha mzigo kwenda UK. Ile kusachiwa akakutwa na uraia wa Uingereza, nikidhani kwa vile rekodi zote wanazo kuwa previously ni Mtanzania, na ameitia aibu Uingereza kukuta na unga, hivyo nilitegemea, Ubalozi ungemtelekeza, but no!, ofisa alitumwa na alihudumiwa huduma zote kama raia kamili wa UK. Wenzetu wanajali.

  Kuna wakati nikiwa mwandishi, nilitelembea ubalozi wetu New York na kule London ukitegemea maofisa watakupokea kwa furaha, i was simply ignored kana kwamba nimekuja kuwachunguza kitu fulani. Hata acess ya kumsalimia tuu balozi, ilikuwa shughul!. Kama japo kusalimia tuu ubalozini ni shughuli, itakuwa kumhudumia mtanzania mwenye shida?.

  Tufikie wakati kwa Mtanzania kupata concern ya Balozi zetu iwe ni right na sio favour, right huwa zinadaiwa, haziletwi kwenye visaani vya chai, tuunganishe nguvu kudai right hizi ili Watanzania nao wawe proud to be Tanzania popote walipo!.

  We wish him to get well soon!.
   
 4. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  pole mgonjwa,pole mleta habari.
   
 5. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Poleni sana
   
 6. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  shukrani pascal kwa inputs zako,nachoweza kusema tu huyu sijui family name yake kwani aliyetuma ujumbe hakusema ila tu ni kwamba anaishi mji wa St.petersburg ambao uko mbali na moscow.Kwa hakika ubalozi ndio unatakiwa umsaidie hata kama hana status na taarifa wanazo.
   
 7. P

  Popov Member

  #7
  Mar 22, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Please specify the full names of the alleged critacally ill Tanzanian in Russia as it may happen to be two or more tanzanians with the same names in Russia.
  If the name is Justin,then there is a tanzanian i know with the same initial in St petersburg(Russia).Provide more details please if any !!
   
 8. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,489
  Likes Received: 5,576
  Trophy Points: 280
  Utanzania kwanza watanzania,kama kuna anaeweza fanya lolote asaidie lakini kama kuna ushahidi wa taarifa ubalozi wetu itabidi wachukuliwe hatua kama mfano
   
 9. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #9
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kweli yupo Mtanzania huyo alioko Hospitalini Jina lake ni Justine Michael na anahitaji msaada wa haraka.Mimi naishi katika mji huu St.Petersburg alipo mgonjwa huyu.Namshukuru mtoa taarifa pamoja na mapungufu yake.Jina kamili la ngonjwa ingawa mtoa taarifa ni wazi analifahamu kwani kama ameweza kuwafahamu wahaya wenzake sidhani kama angelishindwa kufahamu jina la mgonjwa,anuani na namba account na contacts zote kwa watakao taka kumsaidia msaidia mgonjwa ni muhimu.Na mwisho kwa mtoa taarifa na kwa anaedai amemsaidia au anamsaidia mgonjwa katika hali kama hii inapotokea kitu cha kwanza ni kuitisha kikao cha dhalula ukizingatia mtoa habari ni mmoja wa viongozi na kuunda mikakati ya kutatua tatizo lenyewe na sio kulishughulikia individually kuanzia mawasiliano na jamaa zake Ubalozi na kote kunakohusika na kutoa malalamiko kwa WAHAYA,WATANZANIA NA UBALOZI juhudi zako zinapogonga mwamba unakimbilia kutoa lawama.Taarifa uliyoitoa hapa jamvini ikiwa na mapungufu niliyoyataja hapo juu inanifanya niwe na mashaka ya uwezo wako wa kujenga hoja kwa hao uliowasiliana nao kuhusu swala la mgonjwa.Sio wakati wa kutanguliza ukabila ni wakati wakuungana kutatua tatizo hili,mtoa hoja hukuwatendea haki Watanzania wa St.Petersburg.WATANZANIA TULIOPO ST.PETERSBURG HALI NDIYO HIYO TUKUTANANE KUTATATUA TATIZO HILI HARAKA NAMBA YANGU YA SIMU +79216370311
   
 10. i

  itahwa Member

  #10
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kaka umeongea vizuri sana,nilishtuka sana nilipoona mleta habari anaposema wahaya wenzake wamemtelekeza,inamaana kumbe hata mkiwa nje ya nchi bado kaukabila kapo! anyway poleni sana kwa matatizo,inamaana jamaa hana passport au kitambulisho chochote kitakachosaidia kumtambua au email yake au pengine hata simu yake au hata facebook account hii ingesaidia kupata details zake
   
 11. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #11
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Justin Michael | Facebook
   
 12. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kama tukianza kubaguana kwa makabila tukiwa nje ya nchi basi ni hatari kubwa.
  Poleni sana Watanzania mlioko huko, nina amini mtapata ufumbuzi mapema.
   
 13. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2011
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  kAMA JINA LAKE LA PILI NI LA KIHAYA BASI NDIYE HUYO HUYO
   
 14. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Poleni sana
   
 15. S

  Sirikali Member

  #15
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 84
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  kwa hali ilivo ni MUNGU pekee ndiye atakayemuokoa.inasikitisha sana.
   
 16. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Mhm, hali ni ngumu! Ushauri wangu ni kuwa kwa kuwa mgonjwa hana documents za ukazi wake hapo Urusi, hao wenye vibali(Advocate Jasha & Co.) waende ubalozini kushinikiza mgonjwa apewe concern. Kama hao maafisa wa ubalozi ni binadamu lazima watawaelewa, uraia sio makaratasi. Ni mtazamo wangu tu jamani...
   
 17. S

  SELEWISE Member

  #17
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Get well soon...watz mlioko huko msaidieni ndugu...
   
 18. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
 19. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  nchi hii tunalipa kodi zinakwenda wapi kazi zake ndio hizo!!!bwana bado mie nalia na ubalozi huyo ni mtanzania na ndugu zake kama wapo tanzania basi wamsaidie hata kwa kumkopesha ili kuokoa uzima wa jamaa then ndugu zake waje wadaiwe kama wao ubalozi wanaona fedha ni ishu kuliko utu wa jamaa!mie sioni sababu ya ubalozi kugoma wakati wanafunzi tu wana life ngumu na wanamchangie!!!!embu serikali kuweni na utu yanakua kama yale yaliyotokea ukraine miaka ya 2007/2008 kwani kazi za ubalozi ni nini?
   
 20. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hii kitu imenisikitisha sana.
  Lakini pamoja na yote hakukuwa na sababu ya mwanzisha mada aseme eti "Wahaya wenzake wamemsusa" (somthing like that).
  It's not fear.
   
Loading...