Msaada wa haraka kujua dhahabu feki na halisi

TURTEKING

Senior Member
Nov 4, 2020
117
190
Katika pita pita zangu kitaa nikaokota bangili yenye rangi ya gold/ dhahabu niliona kama bati tu ila roho ilisita kuitupa baada ya kuiona Ipo tofauti kidogo Mimi sina ujuzi wowote ule wa kujua dhahabu fake na original
Niliichubua ukutani zaidi ya mara kumi ila ipo vile vile haichuniki wala kubadilika rangi
Naomba mnijuze njia za kawaida kabisa zinazo weza nisibitishia kuwa ni dhahabu fake au original
Nimeshindwa wake picha hapa ..
 
Kwa hisani ya google imesema nyunyuzia kidogo vinegar kwenye hiyo bangili ikibadilika rangi ujue sio gold isipobadilika ni gold. Nina amini zipo tips nyengine
 
Weka picha mkuu,Kuna siku niliokota pete moja nzuri sana mwanza,nzuri saaana nikatatizika kama wewe nikafanya yote hayo ila sikujua,Nilimuonyesha demu wangu wa kipindi kile akaniambia isije ikawa ya majini ,basi ikabidi tuende kwa sonara baada ya siku kadhaa.Ikachovyywa kwenye solution fulani siifahamu,yote ikatoka ile gold coat ikabaki kama bati.Nilichukia sana lakini sikumuonyesha,That ring was very good.
 
Weka picha tafadhali,pia usiivae naona ukienda kukabidhiwa mikoba ya uganga soon,
 
Kuwa nayo makini,maruhani nje nje kwenye hayo mavitu..

Af unashindwaje kuweka picha?
 
Sumaku. Kama una sumaku jaribu kwenye hiyo bangili.dhahabu huwa haigandi kwenye sumaku.ikiganda hiyo sio dhahabu isipoganda ndio
 
katika pita pita zangu kitaa nikaokota bangili yenye rangi ya gold/ dhahabu niliona kama bati tu ila roho ilisita kuitupa baada ya kuiona ipo tofauti kidogo Mimi sina ujuzi wowote ule wa kujua dhahabu fake na original
Niliichubua ukutani zaidi ya mara kumi ila ipo vile vile haichuniki wala kubadilika rangi
Naomba mnijuze njia za kawaida kabisa zinazo weza nisibitishia kuwa ni dhahabu fake au original
Nimeshindwa wake picha hapa ..

Njia ya rahisi zaidi ni kutafuta Acid jitahidi isiwe diluted. Unaidumbukiza hiyo pete. Kama ni dhahabu itabaki kama ilivyo maana sifa ya dhahabu haihathiliwi na acid. Na kama sio dhahabu itasambaratika/kuyeyuka. Imeisha hiyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom