Msaada wa haraka kuhusu Mbeya

popo1986

JF-Expert Member
Jul 30, 2014
1,120
372
Wana body habari zenu wote ..naomba MSAADA juu ya mjini maarufu kwa jina la MATEMA BEACH iliyopo Kyela Mbeya naomba MSAADA wa kuifahamu hyo sehemu
 
Weka sawa bandiko lako unaomba ulekezwe mji wa matema ulipo pale kyela au unataka kujua historia?
 
Mkuu nataka kujua historian na undani sambamba na tamaduni za wenyeji ili niishi Hao vzr
 
Matema beach kama ulivyoandika ni beach ipo ziwa Nyasa wilaya ya Kyela ila sio kyela mjini nje ya kyela zaidi wengine watakusaidia
 
IGWE hebu nijuze kutokea kyela mpaka matema ni sh. Ngapi na ni muda gani? Je? Ni mjini mkubwa ?
 
parefu,sio Chini ya km 60 toka kyela mjini.wenyeji wako poa,wanyaki huwa hatuna matatizo na watu.mvua nyingi sana huko
 
toka kyela ni km 40 nauli kwa sasa inaweza kuwa 20,00-3500 sababu ya mvua hizi,ni sehemu nzuri na kuna huduma zote za msingi
 
Wana body habari zenu wote ..naomba MSAADA juu ya mjini maarufu kwa jina la MATEMA BEACH iliyopo Kyela Mbeya naomba MSAADA wa kuifahamu hyo sehemu

Matema Beach ipo Kyela ni kama 45 kms kutoka Kyela mjini,ila ndugu yangu kwa sasa Matema hakupitiki kutokana na hizi mvua kama unnataka kutembelea Matema Beach ,tembelea wakati wa kiangazi ,kuna hoteli za kitalii ambazohutoza kuanzia kati ya TZs 35000 kwa siku ,kwa vyumba vya kawaida sana na kuanzia usd 60 kwenye vyumba vya hadhi,pia kuna vyumba''mabweni''ndiohivyo 35000 mnachangia choo na bafu,hoteli nzuri ya Blue Canoe imefungwa hadi May katikati hii ni hotel ya mjerumanianaitwa Thomas kamuoa dada yetu mswahili,pia kuna hoteli ya mzungu wa kanisa la pale Mbalinzi anayefuga wanyama pori na mmiliki wa hospitali ya Ifisi pale Mbalizi,pia ipo hotel ya kanisa la Lutheran ambapo pia kuna hospitali ya zamani sana zamani ikiitwa hospitali ya Magareth kama siajkosea,ilijengwa miaka ya zamani sana nadhani kwenye 40s
Usafiri ni wa kuunga unga ingawa kuna basi linaanzia mbeya na kupitia Kyela mjini hadi Matema,ni la kuvizia likipita ndio kwa heri,pia kuna vi Noah vinaanzia njia panda ya kwenda Ipinda ,vinaishia Ipinda ,halafu hapo unaweza kupata vi Noah tena vinavyoenda Matema,au la hasha unaenda Itungi port unapanda meli ya Mbambabay lakini inapitia Matema nadhani ni kati ya Alhamisi au Ijumaa,ila kama nilivyosema hapo mwanzo hata huko Itungi port hakupitiki kutokana na mvua.
Ukitakakuifaidi Matema Beach subiri kiangazi kuanzia August -October .
 
Back
Top Bottom