Msaada wa Haraka Juu ya Subaru Legacy

Hapa hali ndo imekuwa mbaya zaidi wakuu.. saiv ndo haiwaki kabisa na imefifia taa za dashboard zote hazina mwanga hata button ya push to start haiwaki
 
Baba unaweza kubadili battery ila ngoma ikabaki mulemule. Inawezekana alternator hai charge battery vizuri. Kwa ufupi unachopaswa kufanya ni kucheki mfumo mzima wa umeme kwenye gari yako.
 
Mkuu subaru unazijua zijua?maana kuna moja uwa inapoteza nguvu ikiwa kwenye mwendo,ghafla tu gari unaiona inanyata!
Mkuu.... ingawa mimi sio mjuaji sana wa hizi mambo, lakini kuna wakati ninaweza tatua matatizo madogo madogo ya magari.
Naomba nikujibu kama ifuatavyo:-
1. Gari ikiwa kwenye mwendo alafu ghafla ikapoteza mwendo/kukosa nguvu, hapo kitu cha kwanza unapaswa kuangalia Hydraulic pengine imewekwa muda kitambo na labda imechoka hata kupelekea kushindwa kubadilisha gear (hii ni kwa magari ya auto).
2. Kwenye exhaust pana chekeche (filter) ambayo pia kwenye haya magari ya kisasa huwa pengine inaweza ikawa imeziba kutokana na jiko (engine) kuto kuchoma mafuta (oil) vizuri na hivyo kupeleke chekeche la moshi kuziba kwa mafuta (oil).
3. Pia fuel pump ya kwenye tank inaweza ikawa imeziba chujio ama imechoka. Hii pia yaweza kuwa moja kati ya tatizo linalo weza kusababisha gari yako ikose nguvu wakati wa mwendo.

Nina uhakika moja kati ya hayo mambo ndio kwanza unapaswa kuangalia pindi tu pari yako inapo kuwa na tatizo kama ulivyo liahinisha hapo juu.
Nashauri kabla ya kufanya hayo yote, kwanza angalia Air filter na Oil filter kama zipo poa
 
Ahsante sana mkuu,maana kuna mafundi uwa wanafanya kitu rahisi kiwe kigumu ili mradi tu akupige,huu ushauri ushanipa pahali pakuanzia,yan fundi atafuata kile nitakachomuambia kutokana na haya maelezo yako,ubairikiwe sana mkuu
 
Kabla ya kununua battery mpya, kwanza fungua hiyo ya kwenye gari na kisha uipeleke ikapimwe na kisha uichaji.
Ikisha jaa rudi uifunge kwenye gari na kisha jaribu kuwasha mkebe wako.
Baada ya hapo ikiwaka, then jaribu kuondoa tena battery (wakati gari imewaka), na kwakufanya hivyo utaweza baini kama battery ndio imekufa ama otoneta ndio ina shida.
Lakini kama haitowaka baada ya kuichaji, basi jibu litakuwa ni shida kwenye stater.
Hapa hali ndo imekuwa mbaya zaidi wakuu.. saiv ndo haiwaki kabisa na imefifia taa za dashboard zote hazina mwanga hata button ya push to start haiwaki
 
Wakubwa nmefanikisha kuwasha.. naona battery ilkuwa ni tatizo ila sijajua kwanini maana amna kitu niliacha on kwenye gari
 
Basi mkuu n Betri jitaid tembea na waya wa kubust kama ulivosema ukuacha Taa on Mara nying Urudia tena kutokupiga best solution n Betri mpya
 
Asante kwa ushauri.. itabidi nitafute battery nyingine hii hali ikijirudia
 
Wakubwa nmefanikisha kuwasha.. naona battery ilkuwa ni tatizo ila sijajua kwanini maana amna kitu niliacha on kwenye gari
Pole na hongera mkuu.
Sasa hapo patakua na mambo mawili :-
1. Inawezekana moja kati ya nyaya za positive and negative ilikua imelegea.
2. Yawezekana huo ndio mwanzo na dalili ya battery ya gari yako kuanza kufa.

Na kwakua mkebe umepona, ebu nipe location ya bata mkuu...tehteehh
 
Nadhani Battery itakuwa ni tatizo.. basi tukutane kwa Mariam Biriani
 
Back
Top Bottom