Msaada wa Haraka Juu ya Subaru Legacy

Matty96

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
215
194
Wataalamu naombeni msaada wenu juu ya hii gari leo nimejatibu kuiwasha lakini inaishia tu kutoa cranking sound ila haiwaki.. taa za dashboard zinawaka zote lakini taratibu.. hata taa za nje zimepunguza mwanga. Ni Push to start kila nikibonjeza button huku nimekanyaga brake ili niwashe inaishia tu kwenye cranking sound ambayo ni weak sio ile ya kawaida ya kuwasha gari

Nimekwama... Nifanyeje!?
 
Japo si mtaalam sana ila hali inayofanana na kama hiyo ishawahi kunitokea na legacy,mimi ilinizimikia ghafla nikiwa barabarani hadi nikadhani wese limekata but aikua hivyo,baada ya kuangaika sana kuiwasha bila mafanikio nikajaribu kukaza waya za betri,gari ikawaka
 
Nitajaribu kucheza na betri.. inawezekana imepoteza nguvu
Mkuu, battery ikipoteza nguvu maana yake hauna namna nyingine zaidi ya kuipeleka ikachajiwe.
Pia kama battery imepoteza nguvu, hapo maana yake otoneta ilikua haizunguki ili kuichaji battery.
Na kama otoneta ilikua haizunguki, basi maana yake imekata belt ama waya wa main umekatika ama upo lose.
Sasa unacho paswa kufanya ni kama ifuatavyo:-
Kwanza kagua nyaya za positive and negative za kwenye battery kama hakija legea, ukikuta nyaya zimelegea basi zitaiti hata kwa kutumia plaizi na kisha jaribu kuwasha gari yako.
Kama ikikataa, hapo inakupasa utowe battery na ulipeleke likachajiwe na kisha rudi ufunge na kisha washa gari lako.
Kama ikikataa basi hapo ujuwe mkebe wako utakuwa na tatizo kubwa kidogo kwenye either stater ama otoneta
 
Asante Mkuu... itabidi kukikucha nijaribu hizi namna... huku nafanya maombi isiwe shida kubwa kidogo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom