Msaada wa haraka: He loves me he want to leave because I am .....

Logo

JF-Expert Member
Jan 26, 2011
588
48
Wadau nisaidieni, Nina mpenzi wangu ananipenda sana lakini anataka kuniacha sababu mimi huwa ninatatizo la mishipa ya ubongo hunisababishia kutokuelewana vizuri wakati wa mazungumzo.

Daktari yoyote mtaalamu wa masikio, mishipa hapa Dar es salaam yuko wapi anisaidie? nitamuelekeza tatizo langu vya kutosha. Hata hivyo napenda nitoe summury kidogo:-

Huwa nina shida ya kusikia hasa sehemu zenye makelele mengi au mziki mkubwa na kibaya zaidi ninapokuwa na mtu naongea naye nikijihisi tu sisikii basi napoteza yote na siwezi kuelewana naye tena. Help please!
 
Nenda pale EKENYWA Mwembe chai kuhusu kusikia. Nenda family care kwa Dr. Matuja mtaalamu sana wa mishipa ya fahamu.
 
jaman @eny umeandika kifupi mno nipambanulie vizuri niwahi.
 
Nenda pale EKENYWA Mwembe chai kuhusu kusikia. Nenda Family Care kwa Dr. Matuja mtaalamu sana wa mishipa ya fahamu.

Kwenye bold ni majina ya clinic ambazo hao madaktari wanafanya shughuli zao. Hiyo ya pili nafikiri ipo maeneo fulani ya Upanga.

Kutokana na maelezo yako umejita kuwa una;
1. Tatizo la kusikia
2. Tatizo la kupoteza kumbukumbu

Mafanikio katika kuwatafuta madaktari wa kukusaidia.
 
Elekeza vizuri hizo clinic unafikiri huo msaada uliompa unatosha?
 
EKENYWA clinic ipo mwembe chai kwa Shehe yahaya utaona kibao chao na ukiuliza mtu yeyote atakuelekeza tu. na Family Care clinic kwa doctor Matuja ni upanga mtaa wa mfaume au kwa maelezo zaidi ni - PM
 
Ccbrt pale baada ya kanisa la kilutheri msasani kuna hospitali nzuri sana. Wanaweza kukupatia hearing aid kama matibabu yataonyesha uhitaji huo. Hilo la kupoteza kumbukumbu (kama lipo) inawezekana ni kwa sababu ya kutosikia vizuri.

Pole sana. Hebu jali afya yako, achana na huyo mwanamke ambaye anashindwa kukuvumilia. Wenzie wakati wa shida ndo tunashikana haswaa hata kama kuna tatizo unalisahau na kuweka pembeni kabisa. Tibiwa upone, Mungu atakujalia wa kwako mtakaelewana manake hujafa hujaumbika atii.
 
Baada ya kumsoma mtoa mada I was about to say the same. Sijui kama huyo mwanaume ndio anakupa pessure au pressure unajipa mwenyewe ila nadhani afya yako unatakiwa kuijali kwa sababu zako binafsi, sio kulazimishwa na mwanaume. Unaweza invest sana katika kuboresha afya yako na vikashindikana, au kuwezekana, na bado huyo mtu akaendelea na safari yake huko mbele. So do it for you, not for him.
 
kwa sababu umejitambua basi nguvu ya mora itakuongoza katika kushinda mtihani huo, waone wataalam hao na hakika utapata majibu yanayo faaa
 
pole sana kwa kweli. Hata mi nilishawahi kukutana na msichana mwenye matatizo ya kusikia. Kuelewana tabu tupu. Hope utapata matibabu
 
Ccbrt pale baada ya kanisa la kilutheri msasani kuna hospitali nzuri sana. Wanaweza kukupatia hearing aid kama matibabu yataonyesha uhitaji huo. Hilo la kupoteza kumbukumbu (kama lipo) inawezekana ni kwa sababu ya kutosikia vizuri.

Pole sana. Hebu jali afya yako, achana na huyo mwanamke ambaye anashindwa kukuvumilia. Wenzie wakati wa shida ndo tunashikana haswaa hata kama kuna tatizo unalisahau na kuweka pembeni kabisa. Tibiwa upone, Mungu atakujalia wa kwako mtakaelewana manake hujafa hujaumbika atii.

AaCHANE NA MWANAMKE WAKATI YE NI MWANAMKE NA ANAETAKA MKIMBIA NI KIDUME...ACHA KUKARIRI.
 
Back
Top Bottom