Msaada wa fedha kwa anayetaka kwenda kusoma chuo kikuu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa fedha kwa anayetaka kwenda kusoma chuo kikuu.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Msenyele, Apr 27, 2012.

 1. Msenyele

  Msenyele JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tanzania ni miongoni mwa nchi tajiri barani Afrika. Lakini kutokana na mfumo na sera mbaya ya uongozi, siasa na matumizi mabaya ya rasilimali ndicho kinachopelekea watu walio masikini kuendelea kuwa masikini na matajiri kuendelea kuwa matajiri. Ili kujikwamua kuondokana na hii hali, nimepanga kuendelea na masomo cha chuo kikuu katika kitengo cha Information Technology katika chuo kimojawapo hapa nchini. Kwa kuwa bodi ya mkopo inayohusiana na mikopo ya chuo kikuu imejaa urasimu, ningependa kutoa duku duku langu kwa wanajf ili kama kuna kampuni ama taasisi inayosaidia watu wanaojiendeleza kutoka familia masikini mnnijuze ili endapo pengine nitakosa mkopo japokuwa sisemi iwe hivyo, niweze kuwa na njia mbadala ya kuweza kuendelea. Kwa kuwa najiamini katika kila ninachokifanya hasa katika suala zima la elimu kulingana na mazingira husika.Kimsingi niko efficiency more than 90% katika uelewa na kama kuna mtu ana kampuni lake akini sponsor nitakuwa tayari kukubaliana naye kufanya kazi kwake endapo atapenda iwe hivyo. Hata hivyo, mapendekezo ya kusoma course hii si kwamba niko specified na ile ila pia napenda kusoma katika vitengo vya afya kwani nimemaliza form six PCB na sasa hivi namalizia certificate in information technology.

  Ahsanteni wadau niwakaribisha mnipe msaada hata wa mawazo utakuwa msaada mkubwa kwangu.
   
Loading...