Msaada wa dharura: Watoto zaidi ya 600 waliokimbia kukeketwa hawana chakula

Joyce Kiria

Member
Aug 6, 2013
50
109
Wakati watu wengi duniani tukijiandaa kuupokea mwezi wa 12 kama mwezi wa kusherekea sikukuu ya xmas na kufunga mwaka, kule Tarime mkoa wa Mara watoto wa kike wanajiandaa kuzikimbia familia zao ili wasikeketwe. Mwaka huu zaidi ya watoto 600 wapo wamekimbilia kituo cha Masanga ili kuepuka kisu cha ukeketaji. Tuungane kuwasaidia watoto wetu ambao wapo katika hali ngumu hawana maji, chakula, pedi n.k

#TupingeMilaKandamizi

 
Kuwapa chakula na "pedi" hakutamaliza tatizo.

Tuangalie chanzo cha tatizo.
 
Wakati watu wengi duniani tukijiandaa kuupokea mwezi wa 12 kama mwezi wa kusherekea sikukuu ya xmas na kufunga mwaka, kule Tarime mkoa wa Mata watoto wa kike wanajiandaa kuzikimbia familia zao ili wasikeketwe... mwaka huu zaidi ya watoto 600 wapo wamekimbilia kituo cha Masanga ili kuepuka kisu cha ukeketaji... Tuungane kuwasaidia watoto wetu ambao wapo katika hali ngumu hawana maji, chakula, pedi n.k

#TupingeMilaKandamizi

Pamoja na hoja ya kuomba msaada wa Kibinadamu nadhani kilicho bora zaidi na jibu la tatizo kwa haraka zaidi na huko usoni ni kuishinikiza Serikali kuchukua hatua dhidi ya utamaduni huu mbaya na usio wa kibinadamu
Kwamba kwa kuwa tayari tuna mashahidi(Watoto) hatua za kisheria zianze kuchukuliwa dhidi ya hawa Wazazi wa hawa watoto na kama hatua hii inachelewa basi Vyombo vya Habari na Taasisi za Kijamii washikilie bango ya kuwa weka wazi kwa Dunia wazazi wa hawa watoto.
 
Back
Top Bottom