Msaada wa Dawa ya usingizi [ugonjwa wa usingizi]

Mr Finest

Member
Aug 24, 2019
95
103
Wakuu habari za mida
Mimi ni kijana wa 20' age .

Nimepatwa na ugonjwa [matatizo] ya usingizi uliopitiliza, nimekuwa mtu wa kulala Mara kwa Mara pasipo kuchoka, mawazo, depression zozote.

Nikikaa tu kwa kiti, sofa au sehemu yoyote tulivu [Mara chache kwenye kelele] baada ya dakika zisizozidi 2 au 1 kabisa huwa najikuta automatical nalala.

Kwa kweli nikiri limekuwa Ni tatizo kubwa na sugu Sana kwangu nimeanza kujichukia kabisa, familia, ndugu jamaa na maarafiki wamekuwa wakinisema Sana. Mimi mwenyewe nimekuwa nikijitahidi kuondoa tatizo ni mwaka na nusu Sasa nimeshindwa kuondoa tatizo.

Nimejaribu mazoezi na kujiwekea ratiba ya kulala lakini imeshindikana Nimekuja kwenu kuomba kwanza ushauri kwa aliyepitia Kama Mimi amewezaje kutoka kwe ili janga , na pia Kama Kuna dawa naomba msaada wenu [nitaotafuta]

Makabisa maoni na msaada wa mawazo.
 
Nani aliekwambia kulala ni ugonjwa??? Kulala ni afya kijana......kikubwa tu usiji overwork sana kwenye kazi zako za kila siku....
 
Nenda hospitali ukaonane na Dr, medicine haijawahi kuwa rahisi hivyo kwamba kutibiana online?
 
Nenda hospitali ukaonane na Dr, medicine haijawahi kuwa rahisi hivyo kwamba kutibiana online?
Nashukuru kwa mawazo
Kama kuna dawa nadhani utakuwa msaada mkubwa Sana kwangu
Tatizo sisi watoto wa wakulima hatuna BIMA ya kufanya ya hospital
 
 
Usingizi ni mzuri kwa afya ya Akili na mwili mzima kupumzika,ikiwa unalala tu hata wakati umetoka, tafuta shughuli ambayo utaifanya kwa mikono yako ili kuuweka mwili active, Jaribu kunywa na kahawa kavu ambayo haina sukari hii itapunguza usingizi.
 
Niseme kwa upande wangu

Nilikuwa na tatizo kama hilo nikaomuomba MUNGU likatoka kabisa

Nilijichukia sana na kujitukana sana yaaani ilikuwa kila ikifika saa mbili usiku lazima ni lale hatakama nililala mchana

Sema saivi naamua mwenyewe

Kwaiyo kama unataka kuwa kama mimi fanya kama mimi
 
Hilo tatizo la kulala huwa ni la kawaida, na huondoka baada ya muda fulani mwili ukishakomaa physical na mental, hasa baada ya kuanza kupatwa na majukumu ya kimaisha (Maturity Stage).

Na mara nyingi watu wenye tatizo la kulala sana kabla ya kufikia maturity stage huwa wana uwezo mkubwa kiakili "IQ KUBWA SANA", na pindi anapofikia maturity stage tatizo hubadilika kutoka "KUWA ANALALA SANA KUPITA KIASI" na kuhama kuwa "ANAPATA TABU SANA KULALA (HASA NYAKATI ZA USIKU)". Watu hawa ubongo wake hufanya kazi kupita kiasi, anakua mwepesi kuelewa na anakua na akili sana.

NOTE: Tofauti ya "maturity stage (kukomaa kiutu uzima/kukua)" na "puberty stage (kubalee)".

Pia tatizo hili la kulala kupita kiasi linaweza kuwa husababishwa na matumizi ya baadhi ya dawa za binaadamu, uvimbe/jeraha katika ubongo, mishipa ya moyo kuziba.
 
Nani aliekwambia kulala ni ugonjwa??? Kulala ni afya kijana......kikubwa tu usiji overwork sana kwenye kazi zako za kila siku....
Wataalam watatusaidia, nakumbuka kuna kipindi kilirushwa BBC kuhusu ugonjwa wa kulala.Walimhoji mwalimu flan wa Kenya, kiukweli ilikuwa ni tulio la aina yake, yaani teacher ilikuwa akisahihisha daftari mbili tayari usingizi. Alinyimwa hata kuendesha gari, kwani ikiwa hapigishwi story na mtu, ndani ya dakika 2 kashasinzia.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Vipi hali hiyo huwa inaambatana na kujisikia kuchoka sana mwilini muda mwingi au hapana?
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom