Msaada wa dawa ya homa ya manjano

Malakipesa

Member
Sep 24, 2021
41
42
Mdogo wangu wa miaka 14 alikuwa anajisikia vibaya siku mbili hizi sa Leo hajaenda shule nikamcheki usoni akawa wanjano kwenye ule weupe wa macho nikashtuka kikamkimbiza hospital kwa uchunguzi zaidi wakampima maralia hana wakampima nutra sound wakasema tumboni kupo poa.

Mimi nikamwambia dk hii sio dalili za homa ya ugonjwa wa Ini dk akajib hapana hana ugonjonjwa wa ini anadalili za homa ya manjano wakasema nimpe juis ya miwa na ndizi za kupikwa kwa wingi.

Samahanini naombeni wataalamu wa hapa mnijuze huyu mdogo wangu anadalili ya ugonjwa upi? Mana hakuwahi kuwa na tatizo lolote lile hapo awali nawasilisha
 
Mdogo wangu wa miaka 14 alikuwa anajisikia vibaya siku mbili hizi sa Leo hajaenda shule nikamcheki usoni akawa wanjano kwenye ule weupe ...

Hili tatizo linahitaji clinical assessment, ikijumuisha full medical history.. kitu ambacho hatuwezi kukipata humu Jf mpaka uwepo kwenye mazingira ya hospitali na mgonjwa mwenyewe akiwepo.

Hata dawa unazoulizia, ethically hakuna mtaalamu akaeweza ku risk kukutajia.

Njia sahihi zaidi ni wewe kufika na mgonjwa wako hospitali mkuu.
 
Hili tatizo linahitaji clinical assessment, ikijumuisha full medical history.. kitu ambacho hatuwezi kukipata humu Jf mpaka uwepo kwenye mazingira ya hospitali na mgonjwa mwenyewe akiwepo...
Sawa mkuu lakin nilivyoenda hospital dk alikuwa akimuuliza kijana kuwa anajisikiaje kijana alikuwa anamjibu kuwa anachoka halafu anapoteza hamu ha kula muda mwingi analala akaniuliza.

Mimi kuwa mgonjwa amewahi kuumwa ugonjwa wowote kabla nikamjibu kuwa anazaidi ya miaka kumi hajaumwa ndo Mara ya kwanza anaumwa ugonjwa wa aina hii ndo vipimo vikaanza chief
 
Afanye hepatitis panels,hizo dalili zinaonesha ini limepata shida kidogo(acute hepatitis).kwa sasa asitumie dawa za asili au hospitali ovyo bila maelezo ya daktari kwani zinaweza leta shida kubwa kwenye ini.
 
Afanye hepatitis panels,hizo dalili zinaonesha ini limepata shida kidogo(acute hepatitis).kwa sasa asitumie dawa za asili au hospitali ovyo bila maelezo ya daktari kwani zinaweza leta shida kubwa kwenye ini.
Nashukuru kwa ushauri kiongozi tupo pamoja
 
Ini ni serious inahitaji umakini zaidi nenda hosp au kwa mtaalamu wa tiba asili wakueleweka aliye karibu naye kukuambia dawa au kukutajia sio sawa ingekuwa umekuja ofisini ingekua sawa sana. Fuata wataalamu walio karibu na wewe kwa haraka sana. Dogo aendelee na masomo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom