Msaada wa bei/mlioko dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa bei/mlioko dar

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Steven Sambali, Feb 4, 2009.

 1. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #1
  Feb 4, 2009
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Wana JF,
  Naomba kwa wale walioko Dar es Salaam au una habari kamili ya bei ya hivi vitu vifuatavyo. Navihitaji haraka sana. Ntaomba iwe bei ya juu ambayo unaweza kuipata ili kutokuanguka katika shida ya kupanda kwa bei.

  1. Bei gani kuweka katangazo kadogo katika gazeti.
  2. Bei gani kutangaza redioni tangazo la dakika 1.
  3. Bei gani kununua komputer (Desktop PC), monitor, keyboard na mouse na kwa hili itakuwa vema kama ntapata anwani ya wauza computer walioko hapo Dar ili niwasiliane nao. Isiwe ya zamani sana au mpya sana. Tuseme kitu kama Inter Duo 1.8Ghz (not intel 2 duo).
  4. Bei ya kutumia internet cafe kwa saa moja kwa mji wa Dar es Salaam. Kama kuna sehemu wana ukumbi wa mkutano (ukiacza Daza yaani UDSM) na humo wana computer na internet basi ni poa zaidi.
  5. Kukodisha chumba cha mkutano tuseme cha watu kama 50 kwa saa matatu katika hoteli ya middle class.
  6. Bei ya ku-print vitu kama Flyers, visiting cards etc

  Thanx in advance.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Vijana hapo bongo, changamkieni hiyo kitu hapo, unaweza kuwa supplier of some items listed!
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kijana, kama members hawakupi ushirikiano wakutosha nakushauri ipeleke hii kwenye thread ya INVISIBLE ''Request what you need'' anaweza kukusaidia!

  Request what you need

  --------------------------------------------------------------------------------

  Books?

  Toutorials?

  Movies?

  Then we can help... Just post your request and we'll help you get it IF POSSIBLE!

  Invisible
   
 4. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #4
  Feb 5, 2009
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Duu, yaani kimya kabisaaaa.
  Labda niseme kuwa nitahitaji kama computer 10 mpya zikiwa na monitors/keyboards zake kabisaa.
  Juu ya hizo vitu kama Flyers, visiting cards etc zitahitajika zaidi ya 10,000. Kwa chumba ni kuwa nitahitaji kuchukua internet cafe nzima kwa siku kadhaa. Hivyo hizo deal zote kwa kweli si hela ndogo. Nahitaji kujua hizi bei kwani kuna jamaa wanataka kuja kufanya project zao kusaidia WAJASIRIMALI hapa Tanzania. Watategemea kuonana na wajasirimali mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza. Hivyo kabla hawajaja, inabidi kwa wakubwa zao waende waonyeshe bei zikoje na hao Maboss wao waweze kugawa hizo pesa na kama kawaida ya Wazungu, au wao au kupitia balozi wao (wizara ya mambo ya nje) watakuja na kutaka kuona hela zao zimekwenda wapi. Hivyo kila kitu kitakuwa na risiti zake kabisa na si mambo ya kitapeli.
  Najua deal kama hili mafisadi wangelitemea mate. Ila kwa watu wa kawaida inaweza kuwa hela nzuri. Niliwapigia COSTECH ila ukumbi wao unafanyiwa matengenezo na haijulikani kama watafungua tena. Kama kuna ukumbi mwingine wenye computer na internet itakuwa safi sanaaa.
   
Loading...