Msaada wa apartment

Mkuu wana apartments kali sana afu bei poa sasa shida yao ulipie kwa card au paypal ukilipia hawana zengwe?

Ukipata yoyote piga simu, ili upate option nyingine ya malipo, na kufanya booking...

Unajua katika Airbnb kuna watu wana nyumba/apartments etc wanazipangisha on short time stays, kwa watu wenye uhitaji wa muda mfupi...

Fanya kudownload app yao...

Screenshot_20211104-192923~2.png
 
Sisi huku uswazi kuna madalali wa vyumba mambo ya apatimenti hatuyajui kwani kiingereza chetu ni cha kuungaunga, jaribu kwenda Namanga wanapouza maua au zile baa eneo la Morogoro stoo.
Kila kitu kina mwenyewe.
Lakini kwakuwa humu wajuaji ni wengi,
Endeleeni kupotoshana tu.
 
Mambo ya kufikia kwa ndugu yalishapitwa na wakati, ndugu wenyewe hamchelewi kuja kuwasimanga ndugu zenu hapa JF.😜😜
Wewe bwana umenena.

Yaani nisiseme mengi ila nimejifunza kwa macho yangu kwa mtu usiende kama uwezo unao tafuta pango lako uwe unamtembelea tu japo kinafki anaweza kulaumu pia.
 
Wewe bwana umenena.
Yaani nisiseme mengi ila nimejifunza kwa macho yangu kwa mtu usiende kama uwezo unao tafuta pango lako uwe unamtembelea tu japo kinafki anaweza kulaumu pia.
Mimi hata nikisafiri mikoani huwa nina bajeti yangu ya hotel,

Mwaka jana nilitembea Arusha kuna ndugu yangu pia ni ndugu rafiki anaishi USA River alinifuata A town hotelini akanipeleka kwake kupafahamu tulikaa kwake tukapata chakula pale baadaye tukaenda bar kula nyama na bia mpaka usiku mkubwa, akaniomba nilale USA River lakini alinilipia yeye hotel sikurudi tena kwenda kulala nyumbani kwake.

Nililala hotel kesho yake asubuhi baada breakfast ya hotel akanifuata kunirudisha Arusha hotel niliyofikia.

Huo ndio utaratibu wangu kwa sasa popote ninapokwenda hata kama nina ndugu nitakwenda kusalimia labda na kula chakula tu kutia baraka, kwanza mimi napenda kuwa huru hasa nikiwa mikoani inakuwa fungulia mbwa hivi.😄😄
 
Kila kitu kina mwenyewe.
Lakini kwakuwa humu wajuaji ni wengi,
Endeleeni kupotoshana tu.
Sijui upotoshaji uko wapi, sehemu nilizozitaja ndiko wanapatikana madalali wa apatimenti ikiwa pamoja na Rose Garden na baa za Kinondoni makaburini, hivyo ndivyo vijiwe vya madalali wa apatimenti.
 
Mimi hata nikisafiri mikoani huwa nina bajeti yangu ya hotel,

Mwaka jana nilitembea Arusha kuna ndugu yangu pia ni ndugu rafiki anaishi USA River alinifuata A town hotelini akanipeleka kwake kupafahamu tulikaa kwak

Huko ni kuharibu pesa tu...Dar karibia kila mtu ana ndugu ukose pa kufikia ukalale hotel, kwanza ndugu zako watakushangaa
 
Huko ni kuharibu pesa tu...Dar karibia kila mtu ana ndugu ukose pa kufikia ukalale hotel,kwanza ndugu zako watakushangaa
Sio kila mtu humu ni mtoto au kijana msela kama wewe. Yaani mzee mzima akajibane chumba cha watoto kwa kaka yake?
 
Huko ni kuharibu pesa tu...Dar karibia kila mtu ana ndugu ukose pa kufikia ukalale hotel, kwanza ndugu zako watakushangaa

Mkuu mambo ya kutegemea kwa ndugu sahv hayapo, kweli ukakae na mke na mtoto kwa ndugu ? Hayo mambo labda mikoani dar sikuhz hakuna hayo mambo kwanza aibu
 
Mimi hata nikisafiri mikoani huwa nina bajeti yangu ya hotel,

Mwaka jana nilitembea Arusha kuna ndugu yangu pia ni ndugu rafiki anaishi USA River alinifuata A town hotelini akanipeleka kwake kupafahamu tulikaa kwake tukapata chakula pale baadaye tukaenda bar kula nyama na bia mpaka usiku mkubwa, akaniomba nilale USA River lakini alinilipia yeye hotel sikurudi tena kwenda kulala nyumbani kwake.

Nililala hotel kesho yake asubuhi baada breakfast ya hotel akanifuata kunirudisha Arusha hotel niliyofikia.

Huo ndio utaratibu wangu kwa sasa popote ninapokwenda hata kama nina ndugu nitakwenda kusalimia labda na kula chakula tu kutia baraka, kwanza mimi napenda kuwa huru hasa nikiwa mikoani inakuwa fungulia mbwa hivi.😄😄
Huo 'ufisi' shekhe🤣
 
Back
Top Bottom