Msaada: Viwango vya kodi kwa bidhaa kutoka nje tununuazo kwa njia ya mtandao

geek jo

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
1,134
1,143
Habari za mchana wakuu,

Naomba msaada kwa wenye uzoefu na kodi za TRA. Nataka kuagiza bidhaa kutoka nje (China) kwa njia ya mtandao (Alibaba). Ni bidhaa tofauti kwa matumizi yangu binafsi ikiwa ni pamoja na nguo za watoto wangu, viatu ,saa za mkononi pamoja na mabegi. Najua mzigo ukishafika kwa njia ya wasafirisha mizigo (Carrier) mfano DHL,POSTA au wengine wowote itanibidi nilipie kodi!
Je kuna maelezo au system yoyote kutoka kwa shirika letu la TRA itakayo niwezesha kujua kiasi Halisi cha kodi nitakayopaswa kulipia kabla sijaagiza hiyo mizigo yangu! Yaani itakayo niwezesha kufanya calculation zangu kama vile ambavyo tufanyavyo tunapo nunua magari japan. Au kwa namna nyingine yoyote ile.

Mwenye maelekezo kuhusu hilo tafadhari anishirikishe ili niweze kutimiza azima yangu hii.

"Lipa Kodi kwa maendeleo ya Taifa Letu"
 
Aisee! niliwah sikia hum kuwa tax inaweza kuwa saw a na gharama uliyonunulia mzigo ( yaan wanaangalia thamani ya mzigo).

wenye uelewa zaidi watakwambia.
msearch mtu humu anaitwa Michael Mkwanzania.
 
Aisee! niliwah sikia hum kuwa tax inaweza kuwa saw a na gharama uliyonunulia mzigo ( yaan wanaangalia thamani ya mzigo).

wenye uelewa zaidi watakwambia.
msearch mtu humu anaitwa Michael Mkwanzania.
Wataangalia Thamani ya mzigo pekeyake au pamoja na shipping cost!!? Naomba ufafanuzi hapo vizuri. Huyo Michael Mkwanzania nimsearch vp nimuulize yeye direct atakuwa na majibu mazuri zaidi??
 
Ingia hapa step-10-nilivyowekeza-laki-moja-hadi-kuanza-kutengeneza-milioni.

Ipo jukwaa la biashara ameanzisha Michael Mkwanzania
 
Ili kujua thamani ya forodha kwa mizigo inayokuja kwa ndege...tunaangalia thamani ya muamala tu yaan gharama ya mzigo, haiangalii freight, ila kwa mzigo unaokuja kwa maji tunaangalia cost+insuaranc+freight
 
Ili kujua thamani ya forodha kwa mizigo inayokuja kwa ndege...tunaangalia thamani ya muamala tu yaan gharama ya mzigo, haiangalii freight, ila kwa mzigo unaokuja kwa maji tunaangalia Samahani mkuu sija kupata vizuri naomba nifafanulie?
 
Back
Top Bottom