Msaada: Utaratibu wa kufungua kiwanda Tanzania

Walnut Creek

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,622
5,876
Moja ya ndoto kubwa ya Rais Magufuli ni kuwa na Tanzania yenye viwanda. Je kwa vijana wenye ndoto za kufungua viwanda vyao viwe vya bunduki, kemikali, magari,nguo, vyakula na vinginevyo wanahitaji kupitia taratibu zipi za msingi ilikupata leseni, mikopo na misamaha ya kodi ili nchi hii iwe na matajiri wazawa watakaoleta mabidiliko ya uchumi kwenye nchi yao kama wakina Rothschild, Dupoint, Rockefeller, Vanderbilt, Astor na wengine waliofanya Marekani iwe nchi tajiri. Karibuni.
 
Mkuu Tanzania ya viwanda haiwezekani hadi watawala wabadilike nia na kufanywa upya mioyo yao.
Wanataka nchi ya viwanda huku wabunifu hawawezeshi na mara nyingine wanafungwa mfano watengeneza silaha badala ya kuwakusanya na kuwawezesha.
Kuna vikwazo vingi mno hadi kufungua viwanda nchi hii.
Ni wajasiria mali wangapi wamebuni vitu ambavyo ni mwanzo mzuri wa kuwa wazalishshaji bora kesho?
Nchi hii imelaaniwa nfio maana inakumbatia wawekezaji uchwara wa kigeni
 
Mkuu naelewa kuna ugumu kwenye kuanzisha viwanda kwasisi wazawa ndio maana nimeweka hii thread kupata mawazo au ushauri kwa wachache waliofanikiwa au hata kujaribu kuanzisha viwanda hapa nchi ilitupate uzoefu. Naamini tukianza kujadili kuna wengine kati yetu watadhubuti na kufanikiwa.
 
Moja ya ndoto kubwa ya Rais Magufuli ni kuwa na Tanzania yenye viwanda. Je kwa vijana wenye ndoto za kufungua viwanda vyao viwe vya bunduki, kemikali, magari,nguo, vyakula na vinginevyo wanahitaji kupitia taratibu zipi za msingi ilikupata leseni, mikopo na misamaha ya kodi ili nchi hii iwe na matajiri wazawa watakaoleta mabidiliko ya uchumi kwenye nchi yao kama wakina Rothschild, Dupoint, Rockefeller, Vanderbilt, Astor na wengine waliofanya Marekani iwe nchi tajiri. Karibuni.

Umeangalia ile documentary ya...the men who built America ambayo inaeleza walivyo jenga uchumi marekani
 
U
mkuu yani umepewa jina la documentary vizuri kabisa bado unadai link?
wewe ni mgeni wa youtube?
au huijui kabisa?
jifunze kuangalia videos mbalimbali via youtube, sio hiyo tuu...
gonga www.youtube.com kisha search kitu chochote pale.. jifunze leo
Pilau la Eid limenichanganya kidogo naona kuna episodes nne nitazidownload na torrent. Nashukuru sana mkuu kwa kunistua.
 
Kasome kampani act itakupa procedure zote kama utashndwa nenda kwa lawyer yeyote atakusaidia
 
Inawezekana sana kuwa na kiwanda. Kitu muhimu ni kuamini kuwa inawezekana kwa kumtanguliza Mungu. Cha pili ni kuwatafuta Wizara ya Viwanda na Biashara. Watakupa maelekezo mazuri.

Ila sasa na wewe usiwe mwepesi kukubali kila unachoambiwa. Sasa hapo juu kuna mtu amekurupuka na kusema haiwezekani halafu wewe nawe unakubali eti haiwezekani.
 
Mkuu Tanzania ya viwanda haiwezekani hadi watawala wabadilike nia na kufanywa upya mioyo yao.
Wanataka nchi ya viwanda huku wabunifu hawawezeshi na mara nyingine wanafungwa mfano watengeneza silaha badala ya kuwakusanya na kuwawezesha.
Kuna vikwazo vingi mno hadi kufungua viwanda nchi hii.
Ni wajasiria mali wangapi wamebuni vitu ambavyo ni mwanzo mzuri wa kuwa wazalishshaji bora kesho?
Nchi hii imelaaniwa nfio maana inakumbatia wawekezaji uchwara wa kigeni

Kuna mtu anaitwa Dk.Mwaka, mtaani anazungumzwa vizuri na kina mama lakini siku moja aliingizwa msukosuko na serikali mpk nikashindwa kuelewa tunaelekea wapi. Kuna kawaida moja ya binadamu kuhusu itikadi...humponza au kumsaidia. Kuna watu huwaona wenzao threat lakini watu hao hao wakaonekana resource na wengine.

Mimi ningekuwa ndio MAMLAKA, nisingeangalia huyu jamaa kakosea wapi au anakosea wapi, badala yake ningetafuta ukweli juu ya yale yanayosimulika juu yake...simaanishi ukweli wa maneno, hapana ningetafuta concrete evidence kama ni kweli wagonjwa wake hupona. Ingethibitika wanapona au hata kupata nafuu, ningetumia mamlaka niliyonayo kumuhamishia kwenye taasisi za utafiti ili awe tija kwa taifa. Hii ndio namna wenzetu wanafanya na sio majungu majungu. Haya sasa, baada ya sakata loooote lile, kama huyu mtu ni feki, mbona bado kaachwa aumize wananchi?
 
Inawezekana sana kuwa na kiwanda. Kitu muhimu ni kuamini kuwa inawezekana kwa kumtanguliza Mungu. Cha pili ni kuwatafuta Wizara ya Viwanda na Biashara. Watakupa maelekezo mazuri.

Ila sasa na wewe usiwe mwepesi kukubali kila unachoambiwa. Sasa hapo juu kuna mtu amekurupuka na kusema haiwezekani halafu wewe nawe unakubali eti haiwezekani.
Jana ulipoweka uzi wako hapa sijui ununue gari gani, ulishindwa nini kuwatafuta CMC na Toyota wakakueleza kuhusu magari ya sh milioni 23 badala yake ukaleta hapa?
 
Kinachotuponza nchi hii ni ubinafsi, nadhani mwalimu angelizungumzia nalo enzi za hotuba zake ingewapasha akili hawa watawala wetu
 
Kasome kampani act itakupa procedure zote kama utashndwa nenda kwa lawyer yeyote atakusaidia
Nashukuru, hii thread nimeiweka makusudi kupata pia maoni ya watu waliofanikiwa au kujaribu kuanzisha viwanda ilinijue changamoto zake. Jamiiforum si darasa? mimi natafuta elimu hapa.
 
Kuna mtu anaitwa Dk.Mwaka, mtaani anazungumzwa vizuri na kina mama lakini siku moja aliingizwa msukosuko na serikali mpk nikashindwa kuelewa tunaelekea wapi. Kuna kawaida moja ya binadamu kuhusu itikadi...humponza au kumsaidia. Kuna watu huwaona wenzao threat lakini watu hao hao wakaonekana resource na wengine.

Mimi ningekuwa ndio MAMLAKA, nisingeangalia huyu jamaa kakosea wapi au anakosea wapi, badala yake ningetafuta ukweli juu ya yale yanayosimulika juu yake...simaanishi ukweli wa maneno, hapana ningetafuta concrete evidence kama ni kweli wagonjwa wake hupona. Ingethibitika wanapona au hata kupata nafuu, ningetumia mamlaka niliyonayo kumuhamishia kwenye taasisi za utafiti ili awe tija kwa taifa. Hii ndio namna wenzetu wanafanya na sio majungu majungu. Haya sasa, baada ya sakata loooote lile, kama huyu mtu ni feki, mbona bado kaachwa aumize wananchi?
Inasadikika ilikuwa ugomvi wa vimwana, mwak anakula kilain wengine wanasota bila mafanikio...tuache hayo but tunahitajiki kiongozi atakayeona vipaji vya watu wake na avigeuze fursa ya kuleta maendeleo au hata kuwawezesha kuwa wazalishaji wakubwa..viwando vitawezekana.
ATC Arusha wanaunda chopa, cjui huko nyanda kusini wameunda na cjui wamesha chopa kama ni kweli, kwani serikali isione umuhim wa kuwawezesha kwa kuwapeleka vyuo vya wenzetu ili wakirudi wawe waalimu na kudimalia uzalishaji?
Naskia japani waligharamia vijana 100 kwenda mafunzo usa kujifunza uundaji wa magari, leo tunaona TOYOTA imeshika soko duniani.
Vietnam walituma vijana tz kujifunza kilimo cha korosho, leo ni wazalishaji wakubwa korosho duniani.
Raisi na viongozi wafungue maskio na macho yaone umuhimu wa kuifanya tz ya viwanda
 
Nashukuru, hii thread nimeiweka makusudi kupata pia maoni ya watu waliofanikiwa au kujaribu kuanzisha viwanda ilinijue changamoto zake. Jamiiforum si darasa? mimi natafuta elimu hapa.

Cheki hizo episode alafu utaona kama hujachukia UJAMAA maisha yako yote.......Capitalism inatajirisha wachahche lakini wenye smart Ideas wanaweza kujoin ranks za hao matajiri.

Viongozi wa nchi yetu akiwemo mtukufu magu na yeye anawaaminisha watanzania kuwa matajiri ni Evil wakati hakuna hata kiongozi mmoja mwenye akili robo ya mfanyabiashara.

Moja ya ndoto kubwa ya Rais Magufuli ni kuwa na Tanzania yenye viwanda. Je kwa vijana wenye ndoto za kufungua viwanda vyao viwe vya bunduki, kemikali, magari,nguo, vyakula na vinginevyo wanahitaji kupitia taratibu zipi za msingi ilikupata leseni, mikopo na misamaha ya kodi ili nchi hii iwe na matajiri wazawa watakaoleta mabidiliko ya uchumi kwenye nchi yao kama wakina Rothschild, Dupoint, Rockefeller, Vanderbilt, Astor na wengine waliofanya Marekani iwe nchi tajiri. Karibuni.

Rockefeller ni Tajiri wa banking na utajiri wake ulitokana na speculation kipindi cha Napoleon akiongoza ufaransa. Ila hao wengine uliowataja ni matajiri wa viwanda. Dupoint- Mixed Investments, Rockefeller- Standard Oil, Vanderbilt- American Railways, Henry Ford- Ford Motors, Carnegie- US Steel.

Mimi nina ndoto siku moja nione watanzania weusi wanamiliki viwanda vyao wenyewe. Lakini hii itawezekana endapo tutaacha majungu na wivu kwa wengine. Tukipambana inawezekana kuuondoa umaskini wa hii nchi ndani ya miaka 10 peke yake maana china yenye population ya 1billion plus imefuta umaskini kwa 70% ndani ya miaka arobaini, naamini Tanzania yenye population + resources- majungu -wivu - fikra za ujamaa = DEVELOPMENT.
 
Kwa kifupi ni hivi...tanzania ya viwanda haiwezekani ata aje yesu. mpaka,hadi ...............Kuna kama watu hawazidi ata ishirini wakifa hao tutaipata tanzania tunayoitaka iwe viwanda kilimo bora nk.
 
Ni kina nani hao???sidhani kuna tajiri yeyote ninaye ona ana nguvu hapa Tanzania ya kuweza kuzuia maendeleo....Ukipiga pesa kwenye dili zako alafu uwekeze kwenye kiwanda sidhani kama kuna mtu anayeweza kukuzuia
 
Ukitaka kufungua kiwanda kuna utitiri wa taasisi za kiserikali kama TFDA,MANISPAA AU BRELA,TBS NA NEMC yaani utazungushwa hadi utajiona mkimbizi kwenye nchi yako,mimi nina wazo la kufungua kiwanda kidogo lakini nikifikiria izo taasisi hadi napoteza shauku kabisa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom