Ushauri kuhusu biashara ya ushonaji wa nguo na upatikanaji wa vifaa vyake

gpblaze

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
304
14
Naomba anayefahamu mchanganuo wa biashara ya ushonaji wa nguo anisaidie.nataka nione kama naweza kumsaidia mdogo wangu anaweza kushona nguo.sina uwezo mkubwa lakini jaribu kutumia mini quatations.
 
gpblaze,

Kazi ya ushonaji inahiji saana mtu kujituma. Unaweza uwe na mtaji mkubwa saana but asipojituma ni buree... Mtaji wa kushona ndio moja ya biashara unaweza anzia hata nyumbani kama huna pesa ya office ingawa office yapendeza zaidi.

Vitu vya msingi vya kuzingatia (upande wa gharama na ufanisi)

Vifaa:-

A]. Cherehani ya kawaida (line or zig zag) na Cherehani ya finishing.
B]. Vifaa vidogo kama pasi, Mkazi, Nyuzi, Sindano, ki-mashine kidogo cha kugundisha vitu kama stones, maua n.k.
C]. Hivo vipengele [A] & ndizo basics za kuwezesha.

Ya Kuzingatia:-

  1. Kwanza mdogo wako hakikisha kuwa kweli anaipenda hiyo kazi na biashara ya kushona. Maana inaweza ukawa umem direct huko kama njia rahisi ya kuhakikisha kuwa ana kipato kumbe yeye hata haipo moyoni, akilini wala malengoni. Kama hataki unamlazimisha... Hata ugharamie vipi hawezi fanikiwa sababu ni kazi inayohitaji mtu kujituma na kuipenda kazi yake.
  2. Shughuli ya ushonaji imekuwa saana hapa karibuni, inapanuka na kukua kiwango cha heshima juu ya hio sector na Biashara za ushonaji. Hivo inatakiwa ajitume saana kufuatilia nini wengine wanafanya. Ufundi nguo ni moja ya eneo ambalo mtu haachi kujifunza. Kila siku ya Mungu kuna kitu kipya.
  3. Inatakiwa awe mbunifu, mjanja, na makini katika kazi yake. Kuna wateja wengine anaweza ona mshono akataka (maybe ni mnene anataka mshono wa mtu mwembamba); ajue namna ya kujua hii nguo huu yamfaa na kumpendeza, huyu hii itakuwa kituko n.k. Hii inaepusha kutupiwa lawama za kutojua kazi yako. Mwisho wa siku nguo isipopendeza itakuwa kama vile sabb haijashonwa vizuri kumbe mshono kituko.
  4. Ajatahidi saana kutokuwa mroho wa pesa, asiwe mvivu, asiwe msumbufu... Hii yooote itamjengea kuwa na nidhamu katika kazi yake. Kuhakiki ngua inakuwa tayari by deadline, kupanga within range anayoweza mudu (labda nguo zote kuchukua wiki mbili iwe tayari imeisha, na the like)

Mtu ukijipanga vema.... Ushonaji unalipa saana na ni mzuri mradi uwe na malengo na focus ya Biashara yenyewe. Ujue nini unataka, soko lako ni akina nani (akina dada/mama tu? Harusi? n.k); na wanawake wanavaa jamani... Ni moja ya biashara ya uhakika ambayo hulali njaa... Kila la kheri kwa mdogo wako.

Pamoja Saana.
 
Last edited by a moderator:
gpblaze,

Kazi ya ushonaji inahiji saana mtu kujituma. Unaweza uwe na mtaji mkubwa saana but asipojituma ni buree... Mtaji wa kushona ndio moja ya biashara unaweza anzia hata nyumbani kama huna pesa ya office ingawa office yapendeza zaidi.

Vitu vya msingi vya kuzingatia (upande wa gharama na ufanisi)
Pamoja Saana.
umemshauri vizuri sana dada yangu na mungu akubariki sana.
 
habari zenyu wanajf, mi nlikuwa nataka kujiingiza kwenye mambo ya ushonaji, ila sina taarifa juu ya kazi hii. je inaweza kuwa kazi nzuri katika kujiingizia kipato? kwa wanaoijua kazi hii naomba mawazo yenu.
 
Hello!? Mimi ni mkazi wa malimbe mwanza, nina mtaji wa TZS 1,000,000/- kwa ajili ya kufungua duka la ushonaji nguo hapa Malimbe. Naomba ushauri, Je, inatosha hiyo pesa ama niendelee kuiongeza?
Natanguliza shukrani za dhati.
 
Una vifaa na jengo la ofisi tayari au hiyo ndo ya kuanzia kila kitu?
Mimi babu yangu aliwahi kufanya hiyo biashara Dar es salaam maeneo ya tabata, so naweza kumbuka kidogo. Mashine za kushonea kama 3 hivi @ 150,000/=
Mashine ya overlock na kudarizi, sikumbuki bei (tafuta)
Pasi 1 ~ 35, 000/=
Kodi ya eneo ~ 350, 000/=
Picha za mishono ya nguo
Vitambaa vya show ya ofisi
Working capital ya kuanzia ~ 300,000/=
Vifaa vingine vya ushonaji (nyuzi, vifungo, sindano, buttons, zipu, na kadhalika na kadhalika ~ 100,000/=

Ila inategemea unataka uanze biashara yako katika scale gani: ndogo, ya kati au kubwa.
Nakutakia kila la kheri!
 
Hiyo ni yakuanzia kila kitu rafiki yangu!
 
Habarini Wana jamvi ,nataka kujua mkoa ama wilaya hapa Tanzania kwamba nikiwekeza biashara ya ushonaji nguo nitapiga hela
 
Back
Top Bottom