Msaada - Ushonaji


gpblaze

gpblaze

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2011
Messages
304
Likes
0
Points
0
Age
36
gpblaze

gpblaze

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2011
304 0 0
Naomba anayefahamu mchanganuo wa biashara ya ushonaji wa nguo anisaidie.nataka nione kama naweza kumsaidia mdogo wangu anaweza kushona nguo.sina uwezo mkubwa lakini jaribu kutumia mini quatations.
 
AshaDii

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,243
Likes
335
Points
180
AshaDii

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,243 335 180
gpblaze,

Kazi ya ushonaji inahiji saana mtu kujituma. Unaweza uwe na mtaji mkubwa saana but asipojituma ni buree... Mtaji wa kushona ndio moja ya biashara unaweza anzia hata nyumbani kama huna pesa ya office ingawa office yapendeza zaidi.

Vitu vya msingi vya kuzingatia (upande wa gharama na ufanisi)

Vifaa:-

A]. Cherehani ya kawaida (line or zig zag) na Cherehani ya finishing.
B]. Vifaa vidogo kama pasi, Mkazi, Nyuzi, Sindano, ki-mashine kidogo cha kugundisha vitu kama stones, maua n.k.
C]. Hivo vipengele [A] & ndizo basics za kuwezesha.

Ya Kuzingatia:-


  1. Kwanza mdogo wako hakikisha kuwa kweli anaipenda hiyo kazi na biashara ya kushona. Maana inaweza ukawa umem direct huko kama njia rahisi ya kuhakikisha kuwa ana kipato kumbe yeye hata haipo moyoni, akilini wala malengoni. Kama hataki unamlazimisha... Hata ugharamie vipi hawezi fanikiwa sababu ni kazi inayohitaji mtu kujituma na kuipenda kazi yake.
  2. Shughuli ya ushonaji imekuwa saana hapa karibuni, inapanuka na kukua kiwango cha heshima juu ya hio sector na Biashara za ushonaji. Hivo inatakiwa ajitume saana kufuatilia nini wengine wanafanya. Ufundi nguo ni moja ya eneo ambalo mtu haachi kujifunza. Kila siku ya Mungu kuna kitu kipya.
  3. Inatakiwa awe mbunifu, mjanja, na makini katika kazi yake. Kuna wateja wengine anaweza ona mshono akataka (maybe ni mnene anataka mshono wa mtu mwembamba); ajue namna ya kujua hii nguo huu yamfaa na kumpendeza, huyu hii itakuwa kituko n.k. Hii inaepusha kutupiwa lawama za kutojua kazi yako. Mwisho wa siku nguo isipopendeza itakuwa kama vile sabb haijashonwa vizuri kumbe mshono kituko.
  4. Ajatahidi saana kutokuwa mroho wa pesa, asiwe mvivu, asiwe msumbufu... Hii yooote itamjengea kuwa na nidhamu katika kazi yake. Kuhakiki ngua inakuwa tayari by deadline, kupanga within range anayoweza mudu (labda nguo zote kuchukua wiki mbili iwe tayari imeisha, na the like)

Mtu ukijipanga vema.... Ushonaji unalipa saana na ni mzuri mradi uwe na malengo na focus ya Biashara yenyewe. Ujue nini unataka, soko lako ni akina nani (akina dada/mama tu? Harusi? n.k); na wanawake wanavaa jamani... Ni moja ya biashara ya uhakika ambayo hulali njaa... Kila la kheri kwa mdogo wako.


Pamoja Saana.
 
Last edited by a moderator:
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Messages
7,466
Likes
112
Points
160
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined May 21, 2012
7,466 112 160
gpblaze,

Kazi ya ushonaji inahiji saana mtu kujituma. Unaweza uwe na mtaji mkubwa saana but asipojituma ni buree... Mtaji wa kushona ndio moja ya biashara unaweza anzia hata nyumbani kama huna pesa ya office ingawa office yapendeza zaidi.

Vitu vya msingi vya kuzingatia (upande wa gharama na ufanisi)
Pamoja Saana.
umemshauri vizuri sana dada yangu na mungu akubariki sana.
 
AshaDii

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,243
Likes
335
Points
180
AshaDii

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,243 335 180
umemshauri vizuri sana dada yangu na mungu akubariki sana.

I am humbled. Nashukuru Nivea... Mwenyezi Mungu atubariki soote....
 
poul

poul

Member
Joined
Apr 21, 2013
Messages
56
Likes
0
Points
0
poul

poul

Member
Joined Apr 21, 2013
56 0 0
habari zenyu wanajf, mi nlikuwa nataka kujiingiza kwenye mambo ya ushonaji, ila sina taarifa juu ya kazi hii. je inaweza kuwa kazi nzuri katika kujiingizia kipato? kwa wanaoijua kazi hii naomba mawazo yenu.
 

Forum statistics

Threads 1,249,431
Members 480,660
Posts 29,698,250