Msaada/ Ushauri tafadhali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada/ Ushauri tafadhali

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Msindima, Aug 7, 2009.

 1. M

  Msindima JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wanajamii habarini za mchana,
  Nahitaji ushauri wenu katika hili swala limenitatiza sana,mwishoni mwa wiki iliyopita nilipata msiba wa Babu yangu huko kwetu Tanga,na nilipata taarifa jioni ya siku ya jumamosi,nikajiandaa kwa safari kwenda kuwa-join wazazi wangu kwa msiba uliokuwa umetupata,niliwapa taarifa ndugu,jamaa na marafiki kuwa nimepata msiba na jumapili asubuhi nategemea kusafiri ili niwahi mazishi,katika watu amabao niliwapa taarifa ni pamoja na mchumba japo tulikuwa na kamgogoro ka muda mrefu lakini nikaona nimpe taarifa ili asije akasikia kwa marafiki zangu ikaleta shida,nilimtumia sms lakini hakunijibu chochote na ilipofika jumapili asubuhi nilianza safari,mchana kwenye mida ya saa saba ndo nikapokea msg akiniuliza kuwa ni msiba wa nani? na ninakwenda wapi kuzika? nikamjibu ni msiba wa babu yangu na ninakwenda Handeni kuzika baada ya hapo akapiga kimya,lakini nilijiuliza sana kwa nini anyamaze muda wote huo aje aniulize siku ya pili yake,nikaamua kumwuliza jana hukupata msg yangu akaniambia nilipata nikamwambia sawa nikaamua nisiendelee na maswali mengine,nashukuru niliwahi kufika na nikawahi mazishi,na baada ya kukaa huko kwa siku 2 nikarudi maana kazini nilipewa siku 2 tu,kwa kweli wakati narudi sikuona umuhimu wa kumweleza kama narudi kwa sababu hata nilipomweleza nimefiwa response yake sikuifurahia,baada ya kurudi ilipita siku moja na siku ya 2 nilipokea msg toka kwake akilaumu kuwa nasikia tu kwa watu umerudi na ninaelewa kuwa uko mjini na umeshaanza kazi,hiyo kauli pia sikuifurahia nikamwambia hivi wewe hata kuniuliza huko nilikokwenda mambo yameendaje huuulizi unaanza tu kuniambia kuwa unajua niko mjini na sikukwambia kama nimerudi wale ambao ni wa maana kwangu ndo nimewambia nimerudi,kwa kweli nilimwelieza ukweli kuwa sikufurahishwa na jinsi ulivyolipokea tatizo tangu mwanzo kwa hiyo hata wakati narudi pia sikuona umuhimu wa kukueleza kuwa narudi,nilipomjibu hivyo kikazuka kitimtimu huna heshima,una dharau sana,tuachane,nikamwambia kama umedhamiria hayo its fine,nilipomweleza hivyo akaendelea na nitakuja nikushtaki kwa wazazi wako kuwa huniheshimu,nikamwuliza wewe ni kama nani kwangu na kwa familia yangu mpaka uje unishtaki kwa wazazi wangu? na wakati hujajitambulisha na wazazi wangu hawakutambui unaendaje? nilipomwuliza hayo maswali akaanza tena unaona hunithamini,huniheshimu wala hunijali.

  Sasa wadau hebu nisaidieni kosa langu hapo ni nini?
  Ushauri wenu ni muhimu sana,Nawatakia weekend njema!!
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...msindima huna kosa!
   
 3. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Msindima
  Pole sana, hukuwa na kosa. Tatizo ni kuwa mlikuwa na mgogoro wakati umepatwa na msiba japokuwa mchumba wako alitakiwa kuwa na wewe kukupa pole/kukufariji kwa kuweka ugomvi pembeni.
   
 4. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Msindima, baada ya kusoma maelezo yako nimeshindwa kuamini kama huyu ni mchumba kwa matendo yake, hata kama mmegombana kwa vile umepatwa na tatizo tena la msiba alipaswa kuweka yote pembeni na kuona jinsi gani ajihusishe. Sisemi kuwa alilazimika kuja msibani la hasha, angeweza kufuatilia msiba kwa karibu kupitia simu.

  Wewe ndie unamfahamu huyu mtu vizuri na misingi ya relationship yenu. Angalia kama huyu ndie unaetaka kuspend nae the rest of your life. Relationship ambayo inabase kwa mmoja kumbembeleza bembeleza na kumuogopa mwingine ili kuihold hapo kuna kasoro. Ukiona mtu ni mwepesi wa kukutamkia tuachane bila sababu za msingi ujue hapo mguu mmoja ndani mguu mmoja nje so s/he is just looking for an excuse so don’t blame yourself.
   
 5. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Pole Msindima, huyo Bf wako ni wale wanaume wasiojua kujali wapenzi wao.Sasa wewe umefiwa halafu yeye anaonyesha wala hajali vile, na wakati angeweka huo ugomvi wenu pembeni akufariji kwa msiba wa babu, kwa kukutumia sms na hata kupiga simu mara nyingi nyingi.
  Ndio hivyo shost dalili ya mvua ni mawingu na nyota njema huonekana asubuhi. Hivi sasa tu hajaonekana kwa wazazi yupo hivi, akikuweka ndani.....MHHHH! Anyway wewe ndio unamjua zaidi. Hivyo ulivyomfanyia upo right kabisa, wala mie sijaona kosa lako.
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...pamoja na kamgogoro ka muda mrefu, KWANINI mmeng'ang'ania kutumiana sms tu? huduma zote za mazungumzo ya bure kwa simu 'jiachie', 'jirushe' etc hamzitaki? hata kuonana uso kwa uso pia ni ngumu?

  Huna kosa, wote mnamakosa. Jirekebisheni.
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Msindima,
  Dalili ya mvua ni mawingu.
  Wakati wa uchumba ndio wakati wa kutambuana.
  Kosa kama ili na hasira kama hizi wakati wa uchumba mmmhhhhh. Haya hata mkioana yatakuja kuwa hivi hivi tena zaidi ya hivi.
  Jitafutie mwingine.
   
 8. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  msindima pole sana kwa msiba, pili pole wka hiyo hali ya sintofahamu..ninavoona huyo BF wako wala sio mchumba wa kumtegemea,,,ijapokuwa sio kawaida kushauri watu waachane lakini kinga ni bora kuliko tiba...kakma hamtaweza kumaliza tofauti zanu za mwanzo na kama kuna kuwekeana visasi kama hivi, nadhani hakutakuwa na mwisho mzuri. Ulivofanya hujakosea, sema hali hii imetokea mkiwa na kamgogoro tayari. Ushauri ni kuwa kama inawezekana malizaneni kwen hako kamgogoro, kasipoisha basi ujue haikumaanishwa muishi pamoja.
   
 9. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Msindima acha hao wasio jua kupenda,jaribu kuni Pm upate faraja ya kweli.
  Ni dhahiri ana hamu sana ya kuachana na wewe.
   
 10. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  awali ya yote pole kwa msiba.

  naamini ingekuwa vyema kama huyo rafikiyo ungepata japo
  wasaa na kumpigia simu kumueleza habari za msiba. hii mambo
  ya kutumia sms nadhani ulijikwaa hasa hasa ikizingatiwa tayari
  mlikuwapo kwenye mgongano (ambao hujaueleza kiundani).

  inawezekana kwamba mwenzako ametafsiri kumtumia sms kama
  ishara ya mwendelezo wa ugomvi wenu na yeye humuoni kama
  mtu wa karibu kwako aliyehitaji kupewa taarifa hizo za msiba kwa
  kumpigia simu/ana kwa ana.

  kama kweli wampenda mtafute muongee kiutu uzima myamalize.
  sms iweke kando kidogo
   
 11. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Dada pole kwa Msiba!

  Mpige chini! Huyo sii mchumba..tafuta mwingine!
   
 12. M

  Msindima JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu ilinibidi nimtumie sms kwa sababu nilijua fika kwa vile kulikua na mgogoro hata ningempigia simu asingepokea,kwa hiyo ikanibidi nimtumie sms,na pia kuonana uso kwa uso ilikua ni ngumu kwa sababu nimepata taarifa jioni sana na wazazi wangu wanaishi mbali kidogo na ninapoishi mimi kwa hiyo ilinilazimu kwanza kumtafuta mtu atakaekuwa anakuja kuangalia nyumba yangu na ndipo niondoke niende kwa wazazi wangu maana nao hawakuwepo ili nijue kwanza nitasafiri na wadogo zangu wangapi na nani anabaki kule kwa wazazi kwa hiyo kwa mlolongo huo nisingeweza kumtafuta tuonane uso kwa uso.
   
 13. M

  Msindima JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kafara nilishindwa kumpigia simu kwa sababu huwa zinapojitokeza tofauti kati yetu ukimpigia hapokei kwa hiyo nilielewa kuwa nitakapo mpigia asingepokea nikaona njia rahisi nimtumie sms

  Mkuu kumtafuta tuyaongee nashindwa kwa sababu nimechoka na vituko vyake,maana si mara moja kujitokeza haya,hata napokuwa naumwa ukimjulisha wala haonyeshi kujali.
   
 14. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  pole sana kwa mcba mami....mie mwanaume wa kukwaruzana kidogo anarukia neno "tuachane" ananikera kweli...kha
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  umcal ya nini tena kama sms ameipata hajajigusa?....afadhali hata angechelewa kukujibu may b alikuwa mbali na cmu sio hiyo yake ya kujibu kesho yake, ukimnyenyekea man bwana nayo kero....
   
 16. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  pole sana!
  nikikushauri uachane nae nitakuwa siitendei nafsi yako haki,kwa maana umeshapenda.kwa sasa ninaweza kusema VUMILIA TU!mombe mungu.huo ndio msalaba wako
   
 17. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #17
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Pole ila mdogo angu uchumba tu unakuwa hivi? basi ndoa na makwazo yake ataikimbia nyumba na kukuzimia simu, uchumba ni kipindi cha amani, furaha na upendo, hakuna mizigo wala karaha za ndani labda za nje tu.
  Pamoja na yote ninakuonya huu uchumba HAUKUFAI: you as you are, coz wewe na yeye wote mko too proud; hiyo ya "kununiana, kutotembeleana, kuvizia coz asingejibu" shows wewe sio type ya kumbembeleza mtu, so call it a day.
   
 18. M

  Msindima JF-Expert Member

  #18
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kaka naona uvumilivu wangu sasa umefika mwisho,am fade up,naona ni vizuri tu kwanza niamue kutulia na kufanya mambo mengine,huo msalaba sitauweza naona kwangu utakuwa haubebeki.
  Nimejaribu kutafakari sana kwa kina kama sasa hivi hajajitambulisha kwetu mambo yako shaghalabaghala je akijitambulisha itakuwaje? na je tukijakuishi pamoja itakuwaje?
   
 19. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #19
  Aug 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  how old is MR RIGHT?
   
 20. M

  Msindima JF-Expert Member

  #20
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Asante kwa ushauri wako,Mama Joe nilishabembeleza sana vya kutosha na sasa naona imefika mwisho,namwelewa vizuri sana na ndo maana nikasema kuwa inapotokea migogoro huwa ukimpigia simu hapokei,ningefanyeje? any way nitakupm kuna mambo nitakushirikisha i hope utanielewa.
   
Loading...