Msaada unahitajika maana naona kichwa kinaelekea kupasuka

Pole sana ndugu. Dunia hii..... ukifikiri una changamoto kubwa; kumbe wapo wenye changamoto kubwa kukuzidi.
 
Niletee huyo mtoto we pimbi maana nilishawahi muokotaga mtoto ninaye mpaka leo na yupo kidato cha tatu na nampenda na yeye ananipenda sana anajua mimi ndiye mzazi wake.Yaani funza kama nyie hamjui tu watoto ni baraka.
Nimemuwekea na namba yangu kabisa anitafute anipe tumalizane Tena tunaenda kuandikishiana kwa maandishi
Ole wake nilee halafu baadae arudi anamtaka aone ntakachomfanya pimbi kabisa
 
Ukiwa kama mwanaume na hili bandiko lako la kukata tamaa mpaka kufikia hatua ya kutangaza kumgawa mtoto!!kisa maisha magumu kweli?

Hakika kila zama na nyakati zake,vipi ungeachiwa akiwa na miezi 2? Nahisi ungemtupa wewe, itoshe kusema acha uzembe pambana ulee huyo mtoto na ole wako adhulike nitakutafuta na utawajibika,na pengine ndio maana mkeo amekukimbia,sasa kama wewe mwanaume unaweweseka mkeo atafanyaje?
 
Msaada unaitajika ndugu zangu maana hata sijielewi kabisa kwa mambo yanayoendelea. Nilikuwa na mke wangu ila tukaamua kuachana baada ya yeye kuchukua vitu na kuondoka. Baada ya muda kaona haitoshi kamtelekeza mtoto wetu mdogo mwenye umri wa mwaka 1 na nusu kwa sister wangu.
Kwanza kamripoti huyo mwanamke dawati la jinsia na ustawi. Aitwe asemwe na wanawake wenzake kwa akili zake mbovu za kutelekeza mtoto mdogo hivyo.
 
Nilikuwa na wazo kama ilo ila nilivyompeleka kwenye izo day care kila mtu akimuona anataka elfu 50 kwenda juu mi mwenyewe siko vizuri kwa sababu hata kazi muda mwingine inabidi nisiende kwa iyo imeni cost sana kiuchumi
50,000 kwa muda gani?!
 
Shetani akiwa akiwa bize uwa anatuma mwanamke katika majukumu yake mengine.
nilitelekezewa mtoto mdogo 2 years na mtoto si damu yangu, yule bidada akatokomea leo ni miaka 10 na ushee mtoto bado ninae na hakuna anae jua kuwa si mwanangu hata sister anae m- babysit nae hajui kuwa si mwanangu.
sijui siku nikimuambia sister kuwa huyo dogo si damu yangu ata react vipi.
Kama Umeamua kuweka siri na iwe hivyo milele, ukijaribu kuuweka wazi basi usishangae hata huo msaada unaopata sasa ukatoweka au ukamjengea hali ya tofauti na mwanzo kwa huyo mtoto
 
Nipo hapa nawaza ni mwanamke wa aina gani anayeweza kuzaa na kutelekeza mtoto tena mwaka na nusu ameanza na kuita MAMA

Anyway, mtoto hana bibi yake? Au hata kwa dada yako unaweza tafuta msaidizi wa kazi akawa anamuangalia hadi anaporejea toka kwenye biashara zake
Nafikiri hili ni wazo zuri..Sidhani kama anaweza kushindwa kumlipa dada wa kazi.
 
Binafsi nimesoma bandiko la mtoa maada kisha nikasoma comments zote za wadau, halafu nikarudia kusoma tena andiko in a very sympathetic manner, KUSEMA UKWELI, nadhani ambao wametukana au kukejeli na kumdharirisha mtoa maada hawapo fair hata kidogo. Ni bahati mbaya sana daima tunatanguliza empathy yaani kuangalia tatizo la mtu mwingine tukiwa mbali bila kujaribu kuvaa tatizo hilo sisi.

Kuna mtu aliwahi kuandika kwamba, ukiona mtu ameamua kumweka mtoto mtoni/majini basi ujue mtu huyo ameona mtoni ni sehemu salama kuliko nchi kavu. KUTOKA 2:3 Musa aliwekwa mtoni na mama yake akijua ataokotwa na kulelewa.

Mtoa maada ameandika kwa hisia zinazoonyesha anaupendo kwa mwanae na ndiyo maana amesema mda mwingi anashinda naye ila wakati mwingine anatoka kwenda kutafuta riziki hivyo KULAZIMIKA kumwacha mtoto.

Ameomba kama kuna mtu anaweza kumsaidia kumlea mtoto “anaamini” mtoto ni wa jamii nzima ila kama hatapatikana msamaria mwema basi walau awepo wa kumchukua na kumlea kama mwanae ili TU MTOTO AISHI. Huu ni upendo mkubwa kwa mtazamo wangu.

Binafsi nimewahi kupitia changamoto kipindi fulani nikiwa hapo Dar, Mungu pekee ndo anajua, nilijifunza sana na hadi sasa siwezi kumwona mtu mwenye changamoto za kiuchumi kama mzembe na kuanza kumtusi bila kumfahamu in and out.

Huu ni mtazamo wangu tu. HOWEVER, Suala la kumtoa mtoto si kubaliani nalo sana unless that’s the only option left. Nimewahi kufundisha shule sasa kulikuwa na binti wa kidato cha tatu aliyekuja kugundua kuwa alikuwa adopted na wazazi wake hawafahamu, aise japokuwa alikuwa smart form one na two kabla hajafahamu siri hiyo, hali hili ilimwathiri kiasi kwamba kila mmoja pale shule alishangaa jinsi alivyobadilika kutoka mwanafunzi bora hadi kuwa duni wa kwanza darasani.

NDUGU YANGU MUNGU NI MWEMA SIKU ZOTE, NAAMINI KUNA SIKU ATAKUFUNGULIA NJIA NA UTAWEZA KUTOKANA NA CHANGAMOTO HIZO, MWISHO KAMA HUTOJALI NAOMBA UNI PM TUONE NAMNA YA KUSAIDIANA KWA NAMNA YOYOTE.

Aquila non capit muscas!
 
Binafsi nimesoma bandiko la mtoa maada kisha nikasoma comments zote za wadau, halafu nikarudia kusoma tena andiko in a very sympathetic manner, KUSEMA UKWELI, nadhani ambao wametukana au kukejeli na kumdharirisha mtoa maada hawapo fair hata kidogo. Ni bahati mbaya sana daima tunatanguliza empathy yaani kuangalia tatizo la mtu mwingine tukiwa mbali bila kujaribu kuvaa tatizo hilo sisi.

Kuna mtu aliwahi kuandika kwamba, ukiona mtu ameamua kumweka mtoto mtoni/majini basi ujue mtu huyo ameona mtoni ni sehemu salama
Naungana na wewe kabisa. Watu wanahukumu labda huenda hawakupitia hali kama hii. Nililelewa kwa bibi , nilisema siku nitakapokuja kumjua baba yangu nilitamani nikutane na baba masikini sana ili akiniambia alinitelekeza kwa sababu ya ugumu wa maisha walau ningemuelewa.

Lakin siku niliyokutana nae ndo siku niliyomchukia nakujuta kumjua na lau kama si tu Mwenyezi Mungu anataka wazazi wapewe heshima ........ Acha nisiandike nisije nikayajutia. Ila kiukweli mtoa mada Mungu akupe uwezo wa kupambana na kukutoa ktk hili. Bora hata wewe unatfata nani anaweza kukulelea mwanao
 
Pesa hapa ndo tatizo,,sio.

Bora uombe kusaidiwa kwa muda huku wewe ukipambana kutafuta hela uje umlee huyo mtoto hii ya kumgawa mazima haijakaa sawa.
 
Kama mtu huna hela usizae mtoto, dunia ya leo ya kuishi mjini inahitaji shekeli kwenye kila jambo...
 
Back
Top Bottom