Dinatalelee
Member
- Oct 19, 2021
- 8
- 42
Msaada unaitajika ndugu zangu maana hata sijielewi kabisa kwa mambo yanayoendelea. Nilikuwa na mke wangu ila tukaamua kuachana baada ya yeye kuchukua vitu na kuondoka. Baada ya muda kaona haitoshi kamtelekeza mtoto wetu mdogo mwenye umri wa mwaka 1 na nusu kwa sister wangu.
Sister yeye ana biashara zake anazozifanya kwa hiyo muda mwingi yupo kwenye biashara zake pia hapo anapokaa sister kuna barabara, sasa mtoto muda mwingi anakuwa peke yake na kwa vile bado haelewi vizuri unakuta anakaa katikati ya barabara. Mara ya kwanza alishagongwa na pikipiki maeneo hayo hayo ila nashukuru Mungu hakuumia sana ila kibaya zaidi kila siku anakoswakoswa na pikipik au gari.
Sister ameniambia nitafute sehemu nimpeleke maana hapo sio salama kwa mtoto mdogo, huwa najitahidi kushinda nae ila siku nyingine inabidi nitafute hela hata ya kula maana maisha haya kukaa hivi hivi ni ngumu kwa mtoto wa kiume.
Msaada wenu unahitajika jamani, nikipata mtu wa kumpa huyu mtoto anisaidie kunilelea au hata kama akihitaji awe wake basi hamna jinsi maana ni bora mtoto aishi maisha yenye usalama kuliko kuishi maisha ya hatari. Shida kazi yangu ni fundi umeme, ningekuwa hata nauza duka ningeweza kupambana nae.