Msaada unahitajika: Baba anatumia nguvu za giza kulazimisha kurudiana na mama kindoa

Habari za muda huu wakuu, naombeni msaada wenu Mimi ni kijana nilietoka maisha ya hali duni mnoo.

Utotoni nikiandamwa na maradhi na kudhohofu kiafya.

Miaka 15 iliyopita wazazi wangu baba na mama walitengana, wakat nikiwa shule ya msingi ikatokea kutelekezwa, huku, baba akiitelekeza familia na kuondoka huku akituacha peke yetu Mimi na mama.

Hivyo majukum yang yte kimalezi , malazi na mavazi ilikuwa juu ya mama

Nikafanikiwa kupata elimu zte za o-level , A-level hadi stashada ya chuo kikuu mlimani.

Baada ya kumaliza chuo nilimtafuta mzee na kumuomba anionganishe na marafiki zake nipate kazi, hakika mungu ni mwema nikajiria na tasisi moja hapa Tanzania.

Basi nikawa najitahd kubalance kuhudumia baba , mama na ndugu zangu wote.

Changamoto ambayo naipata Kwa sasa ni baba anatak arudiane na mama ili hali mama hayuko tayari.

Mbaya zaidi imefika kipindi Mzee wangu anatumia nguvu za giza kumdhuru mama , ili arud kwake.

Niko njia panda sijui la kufanya naombeni ushaur wenu ktk hali ninayoipitia.

Karibuni
Acha kuitafuta laana, kama kakupigania kazi ukapata kwani we hutaki apiganie ndoa yake irejee? Huoni kwako kuwasaidia wakiwa pa1 ni vizuri kuliko wakiwa wametengana? Lakini pia yaliyomfika baba angalia yasijekukufika au hutaki warudiane? Wazazi waki pa1 raha sana

Ungana na mzee uipate baraka
 
Yafaa wewe Ndio uwe kiunganishi kwa wazazi wako, muombe mama yako akubali kurudiana na baba, you never what happened mpaka mzee akachukua maaumuzi aliyofanya!

Pia usipende sana kudadisi issue za wazazi wako utakuja kuambulia laana toka kwa mmoja wao!
 
Back
Top Bottom