Msaada: Uhamisho wa mwanafunzi wa kike kwenda shule yoyote ya bweni serikalini.

Uzalendo Installer

JF-Expert Member
Nov 8, 2014
5,372
8,839
habari wakuu,
Ninaomba msaada kwa yeyote mwenye uwezo wa kumsaidia jirani yangu (binti) anayesoma shule ya kutwa ya Temeke kidato cha tano aweze kwenda shule yeyote ya bweni ya serikali yenye mchepuo wa EGM kwa sababu mazingira yake ya kusoma ni magumu sana na huyu binti anauwezo mkubwa.
Alimaliza kidato cha nne shule ya sekondari vijibweni na kwa mazingira hayohayo akafanikiwa kufaulu ambapo mimi mwenyewe mwanafunzi ninayesoma Engineering nakiri ningeshindwa kutoboa. Anatoka shule jioni, anafikia kupika na anasoma mda mchache sana usiku. Ninamuombea msaada sababu kidato cha sita asipofanya vizur itabidi arudi kwao Songea ambapo ndipo kuna wazazi wake na hapa dar analelewa tu.
Historia yake ni nzito sana mana unaweza hisi ni hadithi kumbe ni uhalisia.
Natanguliza shukrani kwa yeyote atakaeguswa na kutoa msaada katika hili.
 
Back
Top Bottom