Naomba kuifahamu dawa ya ngiri bila upasuaji

Habari zenu wana-Jf ningependa kupata msaada kwa yeyote anaefahamu dawa ya asili inayoweza kutibu na kumaliza kabisa tatizo la ngiri bila ya upasuaji
Mkuu kuna vitu haviitaji hata uende shule.
Kwanza Ngiri(Hernia) sio Mshipa,

Ngiri maana yake kuna tundu mahala ambalo linaruhusu Utumbo kupenya hilo eneo na kutengeneza uvimbe kwa nje.

Hilo tundu hata ishuke mbingu haitokaa itokee dawa ya kuliziba hilo tundu, lazima likashonwe.

Ni sawa na suruali lako limetoboka afu unatafuta Njia ya kuziba bila kushona...Never and Ever will this ever happen.

Kwa taarifa tu Siku Utumbo ukijibana hapo kwenye hilo tundu ukakosa Damu/Blood supply...Utumbo wote utaharibika/Utaoza na utafanyiwa upasuji mkubwa sana na utumbo utakatwa.

Watanzania tuache ujinga kwa vitu ambavyo haviitaji hata uwe umeenda shule kuweza kuvichanganua.

Ifahamike kuna tofauti ya Ngiri(Hernia) na Ngiri Maji(Hydrocele) ali maarufu kama Busha
 
Kwa jinsi ulivyoelezea apo unafkr mtu ambae ajasoma ata biology atakuelewa aafu unasema kuna mambo ayahitaji ata shule???????
Nguo yako ikitoboka si unapeleka kwa fundi akashone?
Inaitaji kuwa umesoma?

Simple Logic Hernia inatokana na neno la Kiingereza Herniate ni Upenyo/Uwazi kwenye sehemu yoyote ambayo inaruhusu vitu kupenya/kuchepuka iwapo vitu hivyo vitazongwa.

Sasa mtu anataka azibe tundu la suruali kwa dawa za asili
Never seen and Never heard this before...Labda hii inawezekana Sumbawanga huko.
 
Hakuna ugonjwa usio na tiba" mwaka 2012 nilipata ngiri kwenye korodani nikatumia dawa za wamasai mpk Leo hii naickia kwa jirani tu ssa ww unasema haiwez kutibika?
Hiyo haikia ngiri labda hauijui ngiri sio kila kuvimba Korodani ni ngiri
 
Pole sana ndugu yangu Ninayo dawa yakuweza kukutibu ukapona kabisa .tena ntakusaidia bure kabisa njoo pm.
 
Pole sana ndugu yangu Ninayo dawa yakuweza kukutibu ukapona kabisa .tena ntakusaidia bure kabisa njoo pm.
Kama ya kutengeneza , au Kuna majani au mizizi fulani, sema na wengine yaweza kuwawasadia, kipindi hiki Cha barid watu wanasumbuliwa Sana na ngiri.
 
Habari zenu wana-Jf

Ningependa kupata msaada kwa yeyote anaefahamu dawa ya asili inayoweza kutibu na kumaliza kabisa tatizo la ngiri bila ya upasuaji
Mkuu pole sana Dawa ya Asili inayoweza kumaliza tatizo la mshipa wa ngiri pasipo na upasuaji ipo nitafute kwa wakati ili nipate kukutibia upate kona maradhi yako.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom